AfyaMaisha

Umuhimu wa kufanya tendo la ndoa

Sio wengi waojua Umuhimu wa kufanya tendo la ndoa. Wengine hudhania ni zoezi la kufurahisha nafsi Ila tendo hili lipo na manufaa chungu nzima.

Maana ya maneno tutakayotumia kwa lugha ya kimombo

  1. Stress – Mafadhaiko
  2. Stroke – kiharusi
  3. Blood pressure – shinikizo la damu
  4. Prostate cancer – saratani ya tezi

Lazima umewasikia watu kadhaa wakisema ya kwamba kufanya tendo la ndoa kunasaidia sana kwa swala nzima la afya. Kusema kweli hakuna pingamizi kuhusiana na maneno hayo. Lakini wajua kwamba kuwa na mda mwingi na mpenzi wako kunaweza kukakufanya uishi miaka mingi?. Najua unajiuliza vile hii yanawezekana. Naomba uzidi kusoma hapa na nitakuelezea vile haya yote yanawezekana.

Yafuatayo ndio manufaa ya kufanya tendo la ndoa.

Husaidia mwili kupigana na maradhi ( boost immune system)

Kufanya tendo la ndoa kila wakati kunasaidia mwili kuweza kupigana na maradhi mbalimbali. Hii inatokea kwani manake kinga inaongezeka mwilini. Kulingana na utafiti, wanaofanya tendo la ndoa kama Mara moja kila wiki wanaonekana kuweza kujikinga zaidi na maradhi kuliko wanaochukua mda mwingi kabla ya kufanya tendo la ndoa. Hii haimanishi kama wafanya tendo la ndoa, usihau mambo mengine mhimu ya ki afya kama vile kula lishe bora, na kufuatilia chanjo; la lazima pia uzingatie hayo pia.

Hupunguza Mafadhaiko ( Stress)

Tendo la ndoa hutoa chemikali inayojulikana kama oxytocin inayosaidia kupigana na Mafadhaiko ama mkazo wa akili. Kulingana na utafiti, wakati mnapofika kileleni ndio chemikali ya oxytocin huachika. Chemikali hii inayosaidia kupigana na stress. Ukiachilia hii chemikali, unahisi kutulia kwa mwili na hapo ndipo utahisi usingizi na utalala kama mtoto.

Hupunguza maradhi ya moyo

Tendo la ndoa hupungua shinikizo la damu ( blood pressure) na hatari za kuugua magonjwa ya moyo. Unapofanya tendo la ndoa ni kama unaufanyisha moyo wako mazoezi. Tendo la ndoa linachangia kurekebisha mapigo ya moyo na kusema kweli mwenye anafanya mazoezi ya kuendesha baiskeli ama ya kutembea ni sawasawa na anayefanya tendo la ndoa.

Ukiwa na matatizo ya shinikizo la damu alafu ufanye mazoezi husaidia kupunguza tatizo hilo. Bali na kupunguza magonjwa ya moyo, tendo la ndoa pia Hupunguza makali ya ugonjwa wa kiharusi ( stroke)

Hupunguza saratani ya matiti na ya tezi

Kulingana na utafiti, wanaume wanaofanya tendo la ndoa Kati ya miaka 20 mpaka 50, wao wa kupata saratani ya tezi (prostate cancer). Bali na wanaume, kufanya tendo la ndoa hupunguza saratani ya matiti kwa wanawake japo utafiti zaidi bado wafanywa kujua ukweli.

Soma hii pia : faida za maji ya madafu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *