AfyaMaisha

Maji ya madafu na faida zake

Maji ya madafu na faida zake; Kama wewe ni mkaazi wa pwani, basi utakubaliana nami kwamba maji ya madafu Ina umaarufu sana. Wakaazi wa pwani haswa mombasa wanafurahia sana kinywaji hiki.

watalii wakinywa maji ya madafu

Hii sio kwa wenyeji wa pwani tu kwani pia watalii kutoka maeneo mbalimbali hufurahia kinywaji hiki almaarufu kama maji ya madafu. Maji haya hupatikani kwenye nazi ambayo haijakomaa.

Sio kunywa tu bali wakaazi wa pwani hutegemea maji ya madafu ili kupata kipato Cha kila siku kwani kwao ni biashara.

faida za maji ya madafu

Kunao wengi wamefundisha na kuwalea watoto wao na hela wanazozipata kwa kuuza madafu. Mjini Mombasa kwenye barabara tofauti kama vile digo road karibu na marikiti utawakuta wengi sana wakiuza maji ya madafu.

Faida za maji ya madafu.

  1. Husaidia wagonjwa wa presha
  2. Kusafisha figo
  3. Kuongeza nguvu za kiume
  4. Kuifanya ngozi kuwa laini
  5. Husaidia moyo na madini ya potassium
  6. Hushukisha kiwango cha cholesterol

Kusafisha figo

Kulingana na wakaazi wa Mombasa, maji ya madafu huleta tiba aina nyingi. Faida kubwa inayoletwa na maji ya madafu ni kusafisha mwili wa binadamu. Hii sanasana ni kwa upande wa figo na ukizoea kunywa haya maji, basi matatizo ya figo hutoyapata.

Kuongeza nguvu za kiume

Faida nyingine ya maji haya ni kuwa yanasaidia kuongeza nguvu za kiume. Kama tulivyosema hapo awali kuwa maji ya madafu husafisha mwili, basi pia huosha mishipa ya damu na kuifanya damu kutembea bila pingamizi yoyote. Kumbuka kama mishipa yako ya damu haipitishi damu vizuri, Basi itakuwa vigumu uume wako kusimama.

Kuifanya ngozi kuwa laini

Kama ungependa ngozi yako iwe laini basi maji ya madafu inakuhusu. Kulingana na utafiti wetu, wanaotumia maji ya madafu huwa na ngozi laini hata kama umri wako umeenda zaidi. Kumbuka baada ya kunywa yale maji kwenye dafu, pia unaweza pata nazi changa ndani ya madafu. Nazi hii changa inayo madini yanayosaidia ngozi kuwa laini.

Husaidia wagonjwa wa presha

Maji ya madafu pia huwasaidia sana wanawake wazito. Wagonjwa wa presha pia hamujaachwa nyuma kwani ukinywa maji haya presha itashuka. Kulingana na wataalamu wa lishe bora, maji ya madafu ni mazuri ukilinganisha na vinywaji kama soda, juice kwani kiwango chake cha Sukari kipo chini.

Husaidia moyo na madini ya potassium

Wataalamu wa lishe bora wanaendelea kusema kwamba maji haya husaidia moyo na madini ya potassium. Kwenye utafiti mwingine unaosemekana kufanya kumtumia panya, maji haya hushusha kiwango cha cholesterol

Soma hii pia ( chembe cha Moyo na matibabu yake)

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *