Antony Waswa kakake Moses wetangula apumzishwa baada ya kudaiwa kufa na Coronavirus
Ulinzi ulikuwa wa Hali ya juu mchana wa jumatano Kijiji mukhwenya alipozaliwa kakake seneta wa Bungoma Moses wetangula. Ilikuwa ni siku ya huzuni kijijini humo alipozikwa Antony Waswa.
Antony Waswa ambaye ana umri wa miaka 48 alipatana na mauti yake wiki iliyopita jijini Nairobi baada ya madai kuwa aliugua corona

Kabla ya kifo chake Antony Waswa alikuwa msaidizi wa karibu wa kakake mwingine anayejulikana Kama Tim Wanyonyi ambaye ni mbunge wa Westlands. Wengi walitaka kuhudhuria mazishi ya Antony waswa Ila walikatazwa kuingia. Wetangula na kakake wanyonyi walihudhuria mazishi.
Mazishi hayo yalihudhuriwa na watu wasiozidi sitini. Pamoja na waliokuweko ni mwakilishi wa wanawake Catherine Wambilianga kutoka bungoma. Mbunge wa Trans Nzoia Janet Namgabo, mbunge wa Sirisia Jonh waluke na mbunge wa kwanza Ferdinand wanyonyi.
Wengine walikueko ni pamoja na seneta wa Trans Nzoia Michael Mbitoh Bitok na aliyekuwa Mbunge Patrick Wangamati. Shughuli ya mazishi ilichukua mda wa saa moja.