Mchipuko

Betty Kyalo aelezea ni kwa nini alijitoa K24Tv

Ni kwa mda sasa tangu mrembo huyu atoke Media Max’ K24Tv. Wengi wamekuwa wakitaka kujua kitu gani kilifanyika mpaka Betty Kyalo akamua kuacha kazi ya utangazaji. Wengi walisema labda amefutwa kazi japo hawakuwa na uhakika.

Juzi mtangazaji huyu ameamua¬† kuelezea kinaga ubaga wanainchi ni kwa nini alitoka K24 Tv. Haya yote aliweza kuyaongea kwa show ya Online ya Jalang’o inayojulikana kama Bonga na Jalas. Betty alisema hakufutwa kazi kwani jina lake tayari ni kubwa na amelijenga miaka mingi.

K24TV weekend with Betty

“Sikuachishwa kazi K24, Nimefanya kazi kwa bidii sana ili niweze kukuza jina langu. Napenda kazi yangu na huifanya kwa mapenzi kwani najua hii kazi ndio inanipa kipato. Kwa sasa jina langu ni kubwa sana na kila mtu anajua hayo… Nikiona kama natumika huwa najitoa… Alisema Betty”

Betty aliacha kazi K24 mnamo tarehe thelathini mwezi wa may mwaka huu wa 2020. Alipokuwa anaaga watu wakati wa weekend news kwenye K24Tv alikuwa na haya ya kusema…

“Nashukuru kila mtu kwa kwa ile sapoti mmekuwa mkinipa… Nawapenda sana na kwa sasa ni mda wangu wa kutoka ndani ya station ya K24TV.. Mungu awabariki sana hadi tutakapoonana mda mwingine… asanteni…”

Hii inatokea wakati ilisemekana K24Tv wanataka kupunguza wafanyi kazi wake na kuwapunguzia mishahara watakaobakia. Kumbuka Betty Kyalo kabla ya kujiunga na K24 alikuwa anafanya kazi KTN ambapo inasemekana alihamia K24 kwa kupata offer ya hela nyingi.

Soma hii pia, (Tazama hela anayopokea Huddah)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *