Sanaa

Bien wa sauti sol asema hakuamini alichokifanya Size 8

Size 8 ni mzaliwa wa kariobangi south ni mmoja katika familia ya watu saba. Msanii huyu amepitia mengi sana kwa hivyo unapomuona alivyo kwa sasa jua haijakuwa rahisi kwake. Kwa sasa anajulikana afrika nzima na ni msanii mkubwa sana. Size 8 ameolewa na Dj Mo. Dj Mo anafanya kazi NTV na wawili hawa wamebarikiwa na watoto wawili. Bien wa sauti Sol leo ameamua kuwa wazi kuhusiana na Size 8 alichokifanya kabla ya kutoka kwa mziki wa secular music.

Alipomaliza masomo yake ya grade 5-6 katika shule ya upili ya Hillcrest International school, Size 8 alipata chance ya kujiunga na Manchester University lakini hakuwa na uwezo na hapo ndipo alipoamua kujiunga na sanaa ya mziki.

Size 8, Dj Mo and their kid
Size 8, Dj Mo mtoto wao

“Nilikuwa nafanya bidii kwenye sanaa ya Mziki na nilitaka kuwa kama wahu ama Beyonce wa marekani ama Wahu, Wakati nikitazama Beyonce kwenye jukwaa, nilipenda sana alivyokuwa anavalia na wakiti mwingine nilijikuta nanua nguo kama zake ili niweze ku nengua viuno kama yeye. Kama ulikuwa unafuatilia mziki wangu kabla sijaingia kwenye mziki wa injili utagundua kuwa nilikuwa nacheza kama Beyonce…..”

Wakati alikuwa kwenye mziki wa gospel, wengi waliongea mengi kumhusu zaidi yao wakimhukumu kwa lolote lile.

” wakati nilipopata chenye nilikuwa nahitaji, nilianza kuteseka ndani kwa ndani na hata siwezi eleza kwa sasa niliyoyapitia. Cha ajabu ni kuwa, wakati nilikuwa kwenye mziki wa secular sikuwahi kutumia vileo kama vile pombe na vingineo. Nilipokuwa nikiingia kwa pub ama nyumba za starehe, kinywaji changu kilikuwa ni maji tamu ama soda. Nilijaribu kuwa kwenye uhusiano wa mapenzi lakini sikuwahi kufaulu …

Mwanzo mpya wa Size 8

Aliongezea na kusema kuwa hakuwa na marafiki wengi na wenye alikuwa nao hangeweza kuwahesabu kama marafiki wa karibu. Alitamani sana maisha yake ya hapo awali sanasana akiwa shule alipokuwa yuajulikana Linet kabla hajaanza kuitwa size 8. Baada ya Mda, Size 8 amabye jina lake halisi ni Linet Munyali, aliamua kuingia kwenye mziki wa gospel na aliweza kuwaambia watu wawili uamuzi wake. Wawili hao walikuwa dadake Mary na Bien Barasa wa Sauti Sol.

Bien Sauti sol
Bien Barasa Sauti sol

Bien Barasa hakuamini uamuzi wa Size 8 Maana alipokuwa yuajiunga na nyimbo za injili ndio wakati mambo yalikuwa yanamfungukia.

” Alinishangaza sana, alichokifanya ni kama kupewa millioni hamsini alafu uzitupe chooni. Sijawahi kuona ama kusikia mtu yeyote akitoroka pesa…. Haya ndio maneno aliyoyasema Bien.

Haya yote haikumzuia Size 8 Kutojiunga na Mziki wa injili, Uamuzi wake ulikuwa wa mwisho na mpaka saa hii mwanadada huyu bado anafanya mziki wa gospel.

Soma hii pia ( Pesa anayolipwa MCA tricky)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *