Cristiano Ronaldo afunga magoli mawili kwenye.mechi ya Manchester united vs Newcastle
Habari zinapewa kipao mbele ni; Cristiano Ronaldo afunga magoli mawili kwenye mechi Kati ya Manchester united vs Newcastle. Kumbuka Leo ilikuwa mechi yake ya kwanza tangu arudi Manchester united.
Hii ilikuwa mechi iliyongojewa sana na mashabiki wa Manchester united. Wengi walitaka kuona chenye Cristiano Ronaldo angekifanya siku ya Leo.
Wengi walivalia shati zilizoandikwa No. 7 na kila Kona kwenye uwanja wa old Trafford kulionekana shati za Ronaldo. Hii Ina maana sapoti kutoka kwa mashabiki ilikuwa ya hali ya juu huku wengi wakitaka kumuona Ronaldo ambaye ni mshindi Mara tano wa ballon d’ or winner.
Kabla ya Lisaa limoja ndio mechi ianze kulitoka tangazo kwamba Ronaldo angeanza kucheza mechi ya Leo Kati ya Manchester united vs Newcastle. Wengi walionekana kuwa na furaha na hapo ndipo wakaamua kujazika kwenye uwanja wa old Trafford.
Kelele za kumkaribisha Ronaldo zilikuwa kila Kona na nadhani Gwiji huyu alijihisi shujaa. Kumbuka ni miaka kumi na mbili kutokea mchezaji huyu kuhama timu ya Manchester united. Wengi walitaka kujua kama atafunga magoli kama kawaida yake ama la.
Kama kawa, Ronaldo hakuwabwaga mashabiki wake kwani alifunga magoli mawili kwa mpigo.