MaishaMchipuko

Vanessa mdee na Rotimi watangaza uja uzito

Vanessa mdee na Rotimi ambaye ndiye mchumba wake na pia muigizaji wa tamthilia ya power wametangaza uja uzito wao na hivi karibuni watapokea mtoto wao wa kwanza. Habari hizo wamezieka wazi kwenye mitandao na kwa sasa habari imeenea kila sehemu ya dunia.

Vanessa mdee Rotimi

Vanessa mdee na Rotimi walipakia picha zao huku Vanessa akionekana mjamzito na inaonekana imebakia miezi kidogo tu mtoto wao wa kwanza azaliwe na hivi karibuni watakuwa wazazi. Katika mahojiano yao ya hivi majuzi, wawili hawa walisema kuwa mtoto wao atakuwa mvulana.

” Tuna furaha sana na tupo tayari kumpokea mtoto wetu wa kiume. Itakuwa ni Mara yetu ya kwanza kuwa wazazi na hii inamanisha tunapitia mambo mapya kwenye maisha yetu ila tunashukuru na tupo tayari kwa haya matukio….”

Kulingana na Vanessa mdee, safari yake ya uja uzito haijakuwa na changamoto na hajapitia wakati mgumu kama kuumwa na popote pale Ila amekuwa akitamani vitu vya ajabu ama ‘cravings’ wanavyosema wazungu

Kwa mda huu wenye umebakia amekuwa na wakati mgumu kiasi Ila anasema anaelewa maana bado wiki kidogo tu azae. Vanessa anamshukuru mungu kwa zawadi hii

” naweza sema kwamba, hii ni zawadi kubwa sana nashukuru Mungu kwa kutuchagulia hii zawadi.. tuna furaha sana na hii ni heshima kubwa… Aliandika Vanessa mdee..”

Vanessa mdee pregnant

Naye Rotimi kwa upande wake ako na raha isiyokuwa na kifani. Rotimi alisema tokea wanze kuishi na Vanessa mdee maisha yake imebadilika sana na yupo tayari kumfanyia chochote kile ili kumuchunga yeye na mtoto wao

” Wewe ni zawadi kubwa sana kwangu.. umeyabadilisha maisha yangu na kwa sasa tumeungana ili tuweze kumlea mtoto wetu.. naomba mtoto wetu awe na roho kama yako na naahidi kuwa nitawakinga kutokana na Jambo lolote mbaya…” Aliandika Rotimi

Hapa mwangaza news tunawatakia Vanessa mdee na Rotimi maisha mema wanapokaribia kupokea mtoto wao wa kwanza. Mungu awajalie uzazi mwema na wawe watu wa kuelewana maisha yao yote na kusitokee yeyote atakaye kuja Kati yao kuwakosanisha.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *