Maisha

Dua muhimu – umuhimu wa dua hii

Hii ni mojawapo wa dua muhimu na kusema kweli umuhimu wa dua hii umeonekana kwa wengi sana waliyoisema. Ningependa uipitie na bila shaka utapata matunda ya hii dua

DUA MUHIMU
Ewe Mola wangu mimi hakika ni mja wako dhaaifu na wewe ni Mola wangu Latwifu. Sina wa kumlilia zaidi yako Ya Hannan Ya Mannan.

Wewe ndio tegemeo la huzuni zangu na unyonge wangu. Hakika ulimwengu waweza kunitupa lakini wewe daima utaniinua na kunirehemu.

Mola wangu umenihifadhi tangu katika tumbo la mama yangu mzazi hadi leo kufikia kuwa hali nilio. Nakuomba kwenye shari uniepushe na kwenye mazuri uniongoze.

Nikikosa unisamehe na nikipata nitosheke na kuridhika.
Mapenzi yako hakika ni makubwa kwetu Ya Rabbi. Adhabu zako ni kubwa na msamaha wako ni mkubwa zaidi.
Ya Rabbi twalia kwa dhambi zetu na tuko chini ya twaa yako ya Rahmaan.
Ya Rabbi usipotusamehe na kutughufuria hakika tutakua katika hasara.

jinsi ya kuswali
Itakuaje siku ya siku tutakapo simama mbele yako Ya Rabbi na huku tukingoja majibu yetu na kupewa vitabu vyetu.
Hakika hio itakua siku nzito kwetu.
Ya Rabbi tujaaliye kufaulu duniani na akherah.

Ya Rabbi tujaaliye nyoyo zenye kutubu kwa dhambi zetu, nuru katika majumba yetu, huruma kwa wenzetu , ihsaani kwa jirani na waisilamu wenzetu.

Ya Rabbi tujaaliye mwisho mwema sisi na familia zetu.
Ya Rabbi tusamehe dhambi zetu za siri na dhahiri.
Ya Rabbi tujaaliye wema na huruma bayna yetu.

Ya Rabbi tujaaliye kauli njema kwa wenzetu na maneno mazuri bayna yetu.
Kila mkosa Ya Rabbi muongoze na kila mwenye matatizo mpe wepesi.
Ya Rabbi tujaaliye kuwa mbali na fitnah na ubaya.

Ya Rabbi Ya Rabbi Ya Rabbi tujaaliye vizazi vyema .
Ya Rabbi kwako ndio tegemeo la kila mnyonge na mwenye tatizo.
Ya Rabbi tupe muongozo wa dini na tujaaliye kuwa mbali na Jahannamu.
Ya Rabbi Ya Rabbi Ya Rabbi tujaaliye kila la kheri na Tawfiq.
Ameen Ameen

Soma hii pia ( jinsi ya kuoga janaba)

 

 

 

 

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *