Maisha

Ishara za kuonyesha mpenzi wako anatoka nje na mpenzi wa kando

Kuna Ishara za kuonyesha mpenzi wako anatoka nje na mpenzi wa kando

ama ana mchepuko. Kwa wengine huita mpenzi wa nje mpango wa kando. Najua wengi wakati mwingine hutokewa na hisia kuwa wapenzi wao Wana mchepuko. Wengi mpaka leo wametafuta njia za kudhibitisha kama ni kweli lakini utafiti wao haujazaa matunda mpaka sasa.

Nimekuandalia njia tofauti tofauti unazoweza kutumia na ishara za kuonyesha mpenzi wako anatoka nje na mpenzi wa kando. Ningependa kabla hujafanya uamuzi ufanye utafiti mzuri ndio uweze kufahamu kuwa ni kweli mpenzi wako ana mchepuko.

Wajua kama mpenzi wako atakuwa na mchepuko basi jua wewe hautashughulikiwa vilivyo maana mnagawanya mambo mengi na huyo mke mwenza ama mume mwenza.

Huwa ana wasiwasi mwingi Kila Mara

Wakati mwingine ukimwambia mpenzi wako akupeleke sehemu za marafiki wake huonekana na wasiwasi na hutoa sababu nyingi mradi msiweze kutembelea hizo sehemu. Kama basi atakubali muandamane pamoja basi atakuwa na wasiwasi ili usije ukamshika na mchepuko mwenza. Wakati huu maneno humpungukia na hata hutamani chochote kitokee ili muweze kurudi nyumbani.

Wakati mwingine moyo wako husema ukweli.

Kuna wakati unaweza kuwa na mpenzi, haujawahi mshika akiwa na mpango wa kando lakini matendo yake ikafanya umshuku. Hapa ndio tukasema unafaa kusikiliza moyo wako maana wakati mwingine moyo husema ukweli. Mpenzi kama huyu hujirembesha wakati anatoka na kutumia manukato mazuri yasio ya kawaida akidai anaenda kukutana na marafiki zake. Cha ajaabu ni kwamba, wakati unatoka naye huwa hajipambi hata kidogo. Matendo yake huwa ni tofauti na vile umemzoea na hapo ndipo utajua kuna tatizo mahali. Hisia zako zikikwambia mpenzi wa aina hii anatoka nje basi ujue asilimia zaidi ya sitini huenda ikawa ni kweli. Na hapo ndipo unatakiwa kufanya uchunguzi zaidi.

Simu yake ni ya Siri na hataki ushike.

Simu za rununu huficha mengi sana na kizazi Cha sasa kinaweka Siri nyingi ndani ya hizo simu ndio maana Kila mda wanaonekana kwa simu wakichati. Hizi simu zimeongeza udanganyifu sanasana kwa wenye ndoa na pia zimeharibu mahusiano ya watu wengi. Ikifikia hatua kuwa mpenzi wako hataki ushike simu ama hataki uzione chat zake basi huyo mpenzio ana mchepuko. Wengine hawapendi kuweka simu zao moto karibu na wapenzi na kama uko sitting room basi simu yake atapeleka bedroom. Wakati anapoondoka kwenda hata dukani hapo nje, utamuona ataibeba simu yake na kutoka nayo hata kama haendi kuitumia. Wengine wamejaza namba za Siri kwenye app zao Kama vile whatsapp. Yaani huwezi ukaingia kwenye chat zao Kama hujui namba za Siri yaani password.

Humpati wikendi hata kama ni siku ya kupumzika.

Kulingana na kampuni nyingi, wafanyi kazi huwa kazini siku za week days na wikendi huwa ni siku za kumpuzika. Ukiwa na mpenzi alafu ukimwambia mkutane weekend anadai kuwa ameshikika na sio weekend moja ni kila wikendi, basi huyo ana mpenzi wa kando. Kama kweli angekuwa anakupenda wewe angetenga mda wakati hayuko kazini ili muweze ku spend time pamoja. Kama basi atakuwa hapatikani basi jua wewe ni mpango wa kando na kunaye anayepewa mapenzi bila kipimo ndio maana hapatikani siku za wikendi.

Hupost picha na wanaume tofauti.

Watu wengi wakiwa na mchepuko hupenda kumuita kila anayepiga picha naye cousin. Hii huwa ni njia moja ya kuficha uhusiano na huyo mtu anayependa kupiga picha naye huku aki post kwa mitandao. Urafiki wao huwa sio wakawaida na wawili Hawa huwa wanasiri nyingi sana. Mara nyingi wawili hawa hufanya matendo yao kisiri na hata washaelewana watakavyosema kama watakuja shikwa siku moja. Zaidi ya asilimia kubwa ya watu kama hawa huwa hawana uhusiano wowote wa kifamilia na chenye kipo Kati yao ni mchepuko tu.

Hana hisia na wewe yaani hasisimkwi kabisa.

Mwanamke ameumbwa kuwa na hisia tofauti anapokutana na mwanaume anayempenda. Wengine huonekana kuwa na uwoga wa kimahaba na chochote utamwambia hutaka kukifanya ili kukufurahisha. Wakati unapomletea zawadi hulia kwa furaha hata kama zawadi yenyewe ni ndogo lakini kwake huwa ni kubwa kwa kuwa ameletewa na mpenzi wake anayempenda. Basi ukiona mpenzi wako hana shughuli na zawadi zako anaona tu mambo ya kawaida ujue kwamba Hana tena hisia kabisa na wewe. Kuna wanawake wengine hata ukiwakosea wanaona kawaida na hawakuulizi swali lolote sababu ako na mwingine wewe upo tu na hauna faida yoyote kwake.

Hakupatii mawaidha ama changamoto

Mwanamke anafaa kukufaa wakati unapochukua uamuzi kama vile ukitaka fungua biashara anatakiwa awe mstari wa mbele. Anafaa aonekane mwenye kuuliza maswali ili aweze kujua kama umejipanga vilivyo na ikiwezekane aweze kukushauri ili uweze kufanikiwa zaidi. Hii huwa tofauti kwa wapenzi wengine na Mara nyingi utashangaa na wapenzi wengine unapowaeleza unataka kufanya Jambo fulani, wao wanaitikia sawa tu bila hata kuchangia chochote. Hii Ina maana hawana shughuli na wewe. Kama utafanikiwa ama hutofanikiwa ni shauri yako na pia wanakuonyesha chochote unachokifanya uko peke yako. Mpenzi kama huyu huonyesha Hana mda na wewe na roho yake haiko kwako tena.

Marafiki wake wako tofauti

Mara nyingi mpenzi wako anapopoteza hisia na wewe, marafiki zake huwa wanafahamu Kila kitu kinachoendelea Kati yenu. Wengi hutamani waweze kukueleza lakini hawawezi maana kuna Siri kubwa sana washaieka. Marafiki hao hujua mpenzi wako anatoka na nani na kuongezea ni kuwa washapewa Siri zako zote hata za ndani. Basi hao marafiki hukuona bwege na Kila wanapokutazama huonyesha nyuso za huruma. Utajua wazi Kuna kitu kinaendelea maana tabia zao zitakuwa tofauti na walivyokuwa hapo awali.

Soma hii pia ( kwa nini wanawake wanapenda wanaume wahuni)

Hizo ni njia tu kiasi za kuonyesha kuwa mpenzi wako ana mchepuko lakini kabla ya kuchukua hatua yoyote, fanya uchunguzi ili uweze kudhibitisha kama kweli mpenzi wako anatoka nje ama la maana wengine huenda wanaficha simu zao labda usione mambo ya ndani ya familia zao. Wengine hufikiria ukijua kila kitu kuhusu familia zao basi huenda ukamuacha hivo kuamua kuficha simu ili usijue aibu za nyumbani kwao.

Soma hii pia ( jinsi ya kuishi maisha ya raha bila mawazo)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *