AfyaMaisha

Jinsi ya kuishi maisha ya furaha bila mawazo

Jinsi ya kuishi maisha ya furaha bila mawazo

Watu wengi huteseka maishani na sio kuwa hawawezi jikumu ila wamejiekea majukumu mengi. Kunayo machache ningependa kukuelimisha ndio uweze kufahamu jinsi ya kuishi maisha ya furaha bila mawazo.

Yafuatayo ni maelezo ya jinsi ya kuishi maisha ya furaha bila mawazo.

1. Wakati unapowatafutia shule watoto wako, hakikisha kiwango cha ada ya shule kinalingana na uwezo wako. Hakuna haja uzidishe mawazo akilini mwako kila Mara wawaza wapi utapata pesa za kulipa shule ambayo ada yake ipo juu na kuna shule za Bei rahisi. Kumbuka kumpeleka mtoto wako kwa shule ya bei ghali sio hakikisho kuwa atapita mtihani.

2. Kodisha nyumba unayoweza kulipia. Kama kazi yako hailipi pesa za kutosha isijitwike majukumu ya nyumba za Bei ghali. Kuna watu hupata pesa labda kwa wakati flani alafu wakafikiria labda hizo pesa watakuwa wakizipata kila Mara. Watu kama Hawa hukimbilia nyumba za Bei ghali bila kujua hiyo pesa itakuja isha. Ni vizuri kabla hujafanya uamuzi wa kukodisha nyumba, uangalie mwanzo pesa zenye uko nazo kama ni za msimu ama zitakuwepo kwa mda.

3. Wakati mke wako ni mja mzito, jipange vizuri usije ukateseka wakati mtoto atakapozaliwa. Uzuri ni kuwa mtoto huchukua miezi tisa tumboni kabla azaliwe. Hii inamaanisha kuwa kuna mda wa kujipanga na mtu anaweza ekeza pesa mdogo mdogo ndio huo wakati ukifika awe ako vizuri kihela. Pia usisahau watoto ni baraka huenda akizaliwa maisha yako yakafanikiwa na ukapata baraka zaidi.

4. Shida zingine hutokea kwa kutojipanga. Tazama wewe hauna nyumba yako na unajua kuwa mwisho wa mwezi unafaa kulipia nyumba. Hiyo Ina maana kuwa uko na mwezi mzima wa kujipanga na kuekeza pesa ili mwisho wa mwezi uweze kulipia ile nyumba. Usijaribu kuiga maisha ya jirani yako ama rafiki yako. Kumbuka kiwango chenu Cha pesa hakitoshani.

5. Jaribu kuekeza pesa nyingi na ujifunze kutumia hela kidogo. Kumbuka kuna kesho na hujui utakuwa Hali gani. Wakati mwingine kuna dharura ya ugonjwa na kama hujaekeza basi utateseka zaidi. Sio ugonjwa tu, unaweza ukasimamishwa kazi na ujikute hakuna sehemu nyingine unaweza tegemea. Kuna wazazi wengine huwanunulia chakula watoto wao wakati wanaenda shuleni, hiyo haifai kabisa maana chakula Cha kununua kipo ghali kuliko chakula Cha kupika nyumbani.

msongo wa mawazo

6. Wakati mwingine kuna vitu sio lazima kuzifanya maana hazina umuhimu kwenye maisha yako. Kama huna uwezo wa kununua nguo za Bei ghali achana nazo. Usije ukawekeza pesa kwa mda eti ndio uje ununue nguo iko kwa fashion. Kumbuka hamna tuzo za familia yenye kuvaa nguo za Bei ghali. Jambo lingine ni kuhusiana na vyombo vya habari. Sio lazima uwe na DSTV wakati chaneli nyingi zenye zipo kwa DSTV waweza ukazipata kwa GoTv ambayo Bei yake iko chini. Ndio maana nikatangulia kusema achana na maisha ya watu na uishi kama wewe.

7. Kama ni lazima ufanye harusi, basi hakikisha haitakuwa yenye gharama. Sio vizuri uanze kukopa kwa sababu ya sherehe yenye haitakufaidisha na chochote. Ogopa Mungu na uzidi kumuomba alafu hakikisha marafiki wako ni wa maana na wanaweza kukusaidia wakati wa dhiki. Kumbuka kama hauna mpangilio katika maisha basi utaishi maisha ya mawazo na majuto na mwishowe utakuwa na msongo wa mawazo.

matunda na chakula chenye afya

8. Hakikisha unakula chakula chenye afya. Kumbuka ukila vizuri utaepukana na maradhi. Hakikisha unakula matunda ya kutosha ili upate afya nzuri. Pia hakikisha familia yako imelala ndani ya mosquito nets ili Kuzuia maambukizi ya Malaria. Kumbuka wakiwa wagonjwa watahitaki hela ya kugharamia matibabu.

Ni hayo tu kwa leo hapa mwangaza na natumai umejifunza mengi kuhusiana na Jinsi ya kuishi maisha ya furaha bila mawazo. Asante na usisahau ku subscribe kwa kubonyeza kengele nyekundu iliopo pembeni.

Soma hii pia ( jinsi ya Kuzuia Kukoroma usiku unapolala)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *