AfyaMaisha

Jinsi ya kupata mimba kirahisi

Jinsi ya kupata mimba kirahisi

Utakuwa mtu wa kusumbuka sana kama utakuwa haufahamu jinsi ya kupata mimba kirahisi. Kuna wengi wakafikiria labda Wana matatizo ya kizazi ila tatizo ni kuwa hawajafanya uchunguzi jinsi ya kupata mimba kirahisi. Kama hauna matatizo ya kiafya, basi itakuwa rahisi kupata mimba ukizingatia njia nitakazo orodhesha hapa.

Kuna watu hawana tatizo na hili Jambo la kupata mimba na endapo watafanya tendo la ndoa wakati unaostahili basi kupata mimba kwao ni Jambo la kawaida Ila wengine lazima watafute mbinu zaidi. Ifuatayo ni orodha ya mambo unayofaa kuzingatia ili uweze kupata mimba kirahisi.

Style za kupata mimba

Ni vizuri mnapofanya mapenzi, mtumie mtindo mzuri yaani style itakayowezesha mayai kukaa kwa mda ndani ya sehemu ya kike ili kuwezesha urutubishaji wa yai. Wengi tunakosea kwa kutumia mitindo ( styles) zenye huenda sperms zikashindwa kwenda mbali ama pia kumwagika badala kufanya kazi yake.

Mtindo wa missionary position huaminika zaidi na mbegu nyingi (sperms) hupata uwezo wa kupanda mpaka zinakutana na yai ya mwanamke. Missionary position ni wakati mwanaume apo juu ya mwanamke. Epuka kumueka mwanamke juu maana mbegu zitamwagika na zitakuwa hazina maana yoyote. Wakati mnapofanya tendo la ndoa, weka kitu chini ya kiuno Cha mwanamke kama mto hivi ili kiuno kiinuke juu hivo kurahishisha mbegu kuingia ndani bila shida ama kwa urahisi zaidi.

jinsi ya kupima uja uzito

Tushukuru tekinologia maana siku hizi kuna vifaa vinaweza pima mwanamke wakati ako na uwezo wa kupata uja uzito. Kifaa hichi kinajulikana kama ovulation prediction kit. Kifaa hichi kina uwezo wa kujua wakati mwanamke ameengua yai. Kumbuka wakati mwanamke ameengua yai ndio huwa mda mwafaka wake wa kupata mimba akikutana na mwanaume. Kifaa chenyewe kinapatikana kwa duka za kuuza dawa (chemist) na ni rahisi sana kutumia.

Wakati mzuri wa kufanya tendo la ndoa ni kabla ya kuengua yai (before ovulation). Uwezekano wa kupata mimba wakati huu ni asilimia kubwa kuliko kungojea baada ya kuengua yai.

Je, unatamani kupata mimba?

Kama mtakuwa mnatumia ovulation kit, basi itakuwa rahisi kwako maana vipimo vitakaposema kuwa uko positive, basi munaweza kuonana kimapenzi. Kumbuka ovulation hutokea kwa mda wa 48hrs baada ya ovulation kit kuonyesha matokeo ya positive. Hii inamaanisha utakuwa umefanya mapenzi siku mbili au tatu kabla ya ovulation ambapo hapo kuna uwezekano mkubwa sana.

Baada ya hedhi unaweza kupata mimba?

Kulingana na utafiti wa wanasayansi, kutegemea njia za kalenda huenda usipate matokea mazuri. Sababu ni kwamba siku ya hedhi huenda ikibadilika kila Mara kwa wanawake wengi. Kalenda inaweza ikafanya tu kwa wale wanawake wenye mzunguko wa siku 28 ila pia huwezi ukaitegemea asilimia mia. Ni wanawake wengi ambayo sio lazima yai yao iangue baada ya siku kumi na nne. Hii inamaanisha ukitegemea kalenda huenda ukangoja sana bila kupata mimba kirahisi.

Kuna baadhi ya vitu ukizitumia huenda pia zikapunguza uwezekano wa kupata mimba kirahisi kwa asilimia kadhaa. Unapojua wataka kupata uja uzito, lazima upunguze utumiaji wa vitu Kama vile pombe, sigara na pia dawa za kulevya.

Kumbuka kupata mimba ni lazima pia ufurahie tendo la ndoa. Inatakikana matayarisho yenu kabla ya tendo hilo yawe ya hali ya juu na yasiwe ya kawaida kama mlivyozoea hapo mwanzo. Ikiwezekana hata munaweza mkatoka maeneo yenye mumezoea na labda mtafute hata kama ni sehemu tofauti na nyumbani ndio hamu ya tendo la ndoa iweze kuongezeka. Wakati mwanamke ana hamu zaidi ya tendo la ndoa basi husaidia sana kuvuta mbegu za mwanaume ndani ya uke wake na pia mwanaume akiwa na hamu ya kufanya mapenzi, sperms huongezeka hivo basi kuchangia zaidi uwezo wa kupatikana kwa mimba.

mayai ama mbegu za mwanaume, sperms

Kufanya tendo la ndoa Mara kwa Mara pia inachangia uwezekano mkubwa wa kupata mimba. Kulingana na utafiti wa wanasayansi, tendo hili lafaa kufanywa Mara tatu kwa wiki ili kuongeza nafasi ya kupata mimba

Dawa za kusaidia kupata mimba

Kama utakuwa hauna matatizo ya uzazi, basi njia hizo nilizozungumzia zitakusaidia kwa asilimia kubwa sana. Kama bado utakuwa hujafanikiwa, basi itakuwa vizuri umuone daktari, wewe na mpenzi wako ili muweze kufanyiwa vipimo ndio shida ijulikane. Asante kwa kuwa shabiki wa mwangaza news. Tungeomba uweze ku share habari zetu ili ziwafikie wengi.

Soma hii pia ( jinsi ya kuishi maisha mazuri bila mawazo)

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *