Maisha

Kwanini wanawake hupenda wanaume wahuni ama katili

Wengi hujiuliza  maswali mengi Kwanini wanawake hupenda wanaume wahuni ama katili. Wanawake ni viumbe vya ajabu sana maana wengi wao hawapendi wanaume wapole. Sababu ni nyingi sana na Cha ajaabu, wengi wa wanawake Hawa hujiona kwa mikono salama wakiwa na wanaume wahuni na katili.

Unaweza pata mwanamke hupigwa kila Mara na Mume wake lakini bado anachagua kuishi naye. Kila akipewa ushauri aweze kuachana na uhusiano wa mtu kama yule, yeye huona kama anaonewa vile na huchagua kubaki pale pale hata kama Kuna mateso ya hali ya juu.

Hili swala la kwanini mwanamke awe na lazima ya kumpenda mwanaume mhuni halipo tu kwa familia ila pia shuleni hutokea sana. Unakuta msichana mzuri anateswa na boyfriend wake kila siku na Cha ajaabu ni kuwa kuna vijana wengi wapole tena wenye uvuto wanamtaka ila hana mda nao kwani ameamua kubaki na mhuni wake anayemtesa na kumpiga kila siku.

Mara kwa Mara wanawake hawa wanapopigwa na hawa mabwana zao, hurudi makwao na kuapa kutorudi tena kwenye uhusiano ila Cha ajaabu baada ya mda mchache wanarudi na chakushangaza wanaenda kuomba msamaha kwa hao wanaume waliowapiga.

Cause of domestic violence and fight

Tofauti na wanaume, wanawake wengi hawapendi kubadilisha uhusiano kila Mara. Mwanamke akipenda hupenda kweli na huamini atakuwa kwa uhusiano huo mpaka siku yake ya mwisho. Wanawake wengi hupitia mambo mengi sana kwenye mahusiano ila huamua kunyamaza kimya angalau kuficha aibu.

Sababu nyengine inayowafanya wanawake wazidi kukaa na hawa wanaume katili na kuzindi kuwapenda ni kwa masilahi ya watoto. Huenda familia ya mwanamke haina uwezo wa kifedha na mwanamke kama huyu hufahamu wazi kuwa, akiachana na yule mwanaume, watoto wake watateseka. Hapo humlazimu mwanamke yule kuvumulia mateso na kubakia kwenye mateso.

Ni maswali mengi ila kupata majibu ama kuwaelewa wanawake ni vigumu mno. Huenda akaamua kukuchukia ukijidai unampa ushauri mwanamke kama huyu kuachana na mumewe.

Mapenzi ni kitu Cha ajaabu na kila mtu ana sababu ya kukipenda anachokitaka. Kuna msemo husema ni vigumu kuwapa ushauri wapenzi wenye washalala uchi kwa kitanda kimoja.

Soma hii pia ( ishara za kuonyesha kuwa mwanamke anakupenda)

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *