Mchipuko

Familia ya diamond yaandaa sherehe baada ya diamond kuachana na tanasha Donna

Hakuna aliyefikiria kuwa diamond platnumz wangekuja achana na mpenzi wake Tanasha. Wengi walifikiria mapenzi yao yalikuwa ya kufaana na wawili hao wangefunga pingu za maisha.

Kama umekuwa ukifuatilia haya matokeo utakumbuka vizuri kuwa Zari Hassan aliwahi kumuonya tanasha Donna kuwa wakati atapata mtoto atakuja achwa. Wengi hawakulichukulia tamko hilo maanani maana walidhania ni wivu tu Zari ako nao.

Hayawi hayawi mambo yalianza kumuendea mrama tanasha baada ya kusemekana diamond ameanza kumuona mwanamke mwingine. Mwanzo watu walidhania kuwa anataka kurudiana na Hamisa Mobetto Ila tarifa za hapa na pale zimebainisha kuwa diamond ako na mwanamke kutoka nchini Oman anayesemekana ana hela ndefu zaidi na akimpata maisha yake itanyooka zaidi.

Kulingana na vyombo vya habari, Tanasha amevumilia kwa mda  maana mpenzi wake diamond platnumz alianza kumuonyesha dharau kwa mda Ila hakutaka kujulisha watu kwa  kutekuwa alitaka kupigania uhusiano wao. Alipoona hakuna matumaini aliamua kurudi kwao kwani familia ya diamond ilikuwa imeamua.

Juzi familia ya diamond waliweza kukutana kwa sherehe iliyosemekana walikuwa wakisherehekea kuachana kwa diamond na tanasha. Kwa Sasa tunangojea atakaye mrithi tanasha Donna. Je naye atakuja kuachwa ama diamond platnumz atatulia maana inasemekana wembe ni ule ule.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *