Mchipuko

Familia ya Kenei yatoa maneno makali kuhusiana na kifo Cha mwanao

Jana familia ya Kipyegon Kenei ilipata nafasi ya kuutazama mwili wa mwanao Ila walionekana wenye majonzi. Uchunguzi wa kifo Cha Kipyegon Kenei unaendelea huku wengi wakiomba uchunguzi uharakishwe.

Ni Jana tu naibu wa rais alitoa amri kwa kinoti aweze kuharakisha uchunguzi ili wanainchi wajue ukweli akidai kuwa wanainchi wamechoka kuzungushwa.

Kenei alikufa siku kadhaa zilizopita huku sababu tofauti kuhusu kifo chake zikijitokeza. Babake kenei alisema kuwa hawataruhusu waliotelekeleza uovu huo kufaulu bila kupata adhabu. Aliongeza kuwa damu ya kenei itawafuata popote pale wataenda.

John chesang ambaye ni babake marehemu aliomba serikali ifanye uchunguzi wa kina na wahakikishe wahusika wamepatikana.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *