Mchipuko

Gari alilonunuliwa Tanasha Donna lapata umiliki mpya

Mwaka uliopita katika sherehe ya kuzaliwa kwao Tanasha na mamake diamond platnumz walizawadiwa gari Aina ya Toyota Prado. Chakushangaza ni kuwa, Tanasha Donna hakuondoka na Hilo gari walipoachana na diamond platnumz.

Habari zinazotufikia ni kuwa Tanasha hangeruhusiwa kutoka na hilo gari kwani stakabadhi zaonyesha kuwa gari lenyewe limesajiliwa kwa jina la mamake diamond platnumz, Sandra kassim. Kulingana na mwandishi mmoja, magari mengi ndani ya wasafi huwa imesajiliwa kwa jina la mamake diamond na vigumu sana kutoka na gari.

Kwa Sasa Tanasha Donna ako nchini Kenya na anaonekana kuendelea na maisha yake ya kawaida. Familia ya diamond wamedai kuwa hawawezi wakauza hilo gari la Tanasha Donna Aina ya Toyota Prado Ila itabakia kuwa ya familia.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *