Maisha

Grace Ekirapa | Nimewahi kuolewa Mara mbili

Grace Ekirapa Ni mtangazaji mashuhuri na Kama unapenda kutazama runinga ya NTV kila jumapili Basi itakuwa unamfahamu. Yeye na DJ Mo ndio huongoza kipindi Cha crossover kinachopeperushwa kila siku ya jumapili.

grace Ekirapa na DJ Mo

Mwanadada huyu juzi alielezea Uma aliyoyapitia kwenye maisha yake. Amekuwa kwa uhusiano kwa Mara mbili lakini mpaka Sasa hajapata mwanaume anayeweza kufunga naye pingu za maisha. Mwaka wa 2017 alikuwa kwa uhusiano Ila baada ya miaka nne alijikuta kwenye uhusiano mwingine.

 Grace Ekirapa's sisters
Dadazake Grace Ekirapa

Grace Ekirapa alisema kuwa hakuamini kuwa uhusiano wake ungefika kikomo baada kugharamikia. Mrembo huyu alijua wazi ashapata mpenzi ambaye angeishi naye maisha yake yote Ila haya yote hayakufanyika.

beauty queen grace Ekirapa

Baada ya uhusiano wake wa kwanza kuvunjika, grace Ekirapa alijihisi mnyonge na kuchukia mapenzi kwa moyo wake wote. Huu ulikuwa mwaka wa 2017 baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa miaka nne. Badala ya kukaa chini na kufikiria kilichosibu uhusiano wake, Grace Ekirapa aliamua kuingia kwa mapenzi tena

Mwaka wa 2018 ndio mwaka grace Ekirapa alipata mpenzi mwingine. Mwezi wa tatu, mwanadada huyu alifanya harusi ya kitamaduni iliyohudhuriwa na watu Mia nne. Baada ya mda akaanza kujutia uamuzi wake kwani aliolewa na rafiki yake Ila akagundua kuwa hawakuoana sababu ya mapenzi kwani nia yake ilikuwa kujulipishia yaliyomfanyikia hapo awali.

grace Ekirapa na size 8
grace Ekirapa na size 8

Hapo ndipo Grave Ekirapa aligundua kuwa amefanya makosa kwani uhusiano huu hauungepata baraka za mwenyezi Mungu. Alijua yuaumiza mwenzake mwenye hakustahili kuumizwa. Baada ya wiki moja kwenye uhusiano wake wa pili, mambo yalianza kwenda mrama na ikabidi Grave Ekirapa ajitenge na mwanaume huyo aliyekuwa mpenzi wake.

Wakati akiwa amejitenga alimuomba Mungu ampe nguvu ya kumpenda yule mwanaume ama ampe ujasiri wa kumueleza yule mwanaume Kama hampendi.

Nilipata ujasiri na kuamua kumueleza kuwa uhusiano wetu haungeenda mbali. Hapo ndipo uhusiano wao ulifikia kikomo. Wengi walishangazwa na uamuzi wake na kumtukana grace Ekirapa kila Aina ya matusi.

“Nikikaa kwa nyumba kwa mda wa wiki moja. Hakuna aliyenijali kila siku nilikuwa nalia peke yangu kwa nyumba bila kula Wala kupata usingizi..”

Soma hii pia ( uhusiano wa tanasha na Jamal gaddafi)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *