Afya

Habari njema kutoka nchini China

Kama inavyojulikana dunia nzima, hii ndio nchi ilivyokuwa ya kwanza kutangaza uwepo wa virusi vya Coronavirus. Watu nchini humo wamepoteza maisha yao na hii nchi ilirekodi visa vingi sana.

Madaktari nchini humo wamekuwa mstari wa mbele kujaribu kipigana na Coronavirus na wengi wao wamepoteza maisha yao katika harakati hizo kwani wamekuwa wakipatana moja kwa moja na wagonjwa wa homa hiyo.

Naweza kusema bidii yao imezaa matunda kwani ni Kama wamefaulu. Taarifa za hivi punde zasema kuwa nchi ya china kwa mda Sasa hawajarekodi tukio mpya kuhusiana na virusi vya Coronavirus. Hii inamaanisha wameweza kudhibiti homa hiyo.

Makataa ya kutotoka nje imechangia sana kufaulu kwao na wameweza kipigana na virusi hatari. Kwa Sasa nchi yao ipo salama kwani kampuni nyingi zimeanza kuendelea na shughuli zao za kawaida.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *