Mastar wawili tajika wabongo wapatwa na Coronavirus
Leo imekuwa siku ya huzuni nchini Tanzania baada ya wawili hawa kutangaza kuwa na virusi vya Corona.
Wawili hawa ni msanii tajika mwanaFA na meneja mkuu wa diamond platnumz bwana sallam SK. Katika maongezi yake hapo awali, mwanaFA amewahimiza wa Tanzania kutahadhari sana na ugonjwa huu akiwahimiza wanainchi kutumia mapendekezo yanayotolewa na vituo vya afya.
mwanaFA amesema kwa Sasa amejitenga ili kupokea matibabu na familia yake iko salama kwani kutoka atoke Safari, hajakutana na watoto wake. Ameongeza kuwa mashabiki wake wasiwe na wasiwasi kwani hii ni homa tu na baada ya mda mfupi atakuwa sawa
Tunawaombea wawili hawa nafuu ya haraka na bilashaka mwenyezi mungu atawaponya na wataendelea na ujenzi wa taifa
996 total views, 1 views today