MaishaSanaa

Historia ya Christina Shusho

Baada ya utafiti wa kina uliofanywa na timu yetu ya mwangaza news, hatimaye tumeweza kukamilisha mengi yanayohusu Historia ya Christina Shusho. Kama wewe unapenda mziki wa injili basi utakuwa unamfahamu msanii huyu tajika kwa jina Christina Shusho.

Christina Shusho ni mwanamziki wa nyimbo za injili anayeheshimika sana. Anatokea nchini Tanzania na nyimbo zake zinapendwa sana nchini humo na nchi zingine barani afrika.

Mwanamziki huyu ana uwezo mkubwa sana wa kuandika nyimbo za injili na kwa kweli ukisikiza nyimbo zake utakubaliana na Mimi kwamba uwezo wake ni mkubwa sana. Sauti ya mwanadada huyu haiwezi fananishwa na yeyote yule kwani iko kivyake na ni sauti ya kuvutia.

historia ya Christina Shusho

Mziki wa Christina Shusho husikizwa na watu wa umri mdogo na umri mkubwa. Wasanii wengi wameshindwa kuichukua nafasi yake na hii yamfanya abaki kuwa kileleni. Christina Shusho ashawahi kushinda tuzo nyingi sana katika safari yake ya Mziki.

Maisha ya Christina Shusho ilikuwa ya kawaida kwani alianza kama mfanyi Kazi wa kuosha kanisa. Sio wengi walidhania angekuja kuwa msanii wa injili anayeheshimika sana afrika mashariki.

Christina Shusho biography

Kwa mda mwingi, Christina Shusho amekuwa nchini kenya kwa tamasha za mziki na mahubiri. Christina Shusho husema wanamziki wengi chipukizi nchini kenya wanafanya mziki ili wapate jina Ila hawafanyi kwa sababu ya kusambaza injili. Kulingana na yeye, anamtambua sana Mercy Masika kwani yeye hafanyi mziki kwa sababu ya pesa ama fame.

Christina Shusho alizaliwa na kulelewa sehemu inayojulikana kama Kigoma nchini Tanzania. Alisomea shule ya msingi na ya sekodari ya Kigoma.

Wakati akifanya Kazi ya kuosha kanisa, Christina Shusho alipata nafasi ya kujiunga na kwaya ya kanisa hilo. Hapo ndipo ndoto zake za kuwa mwanamziki zilianzia kwani alitamani sana kurekodi nyimbo zake na kuwa mwanamziki wa injili tajika.

Nyimbo yake ya kwanza ilikuwa yajulikana kama “kitu gani kinitenge na upendo wa bwana” nyimbo hii ilipendwa sana nchini Tanzania japo haikuweza kupenya vizuri nchi za kigeni.

Shusho family photos

Album ya pili na ya tatu zilifanya vizuri sana kwenye soko na hapo ndipo jina lake likaanza kujulikana hadi nchi jirani. Nyimbo zilikuwa ni “unikumbuke” na ” nipe macho nione”. Nyimbo hizi zilichezwa sana nchi za kigeni na aliweza kuandaa tamasha nyingi kwani watu wengi walitamani kumuona Christina Shusho kwenye jukwa akifanya mambo yake.

Christina Shusho ako na nyimbo na Ringtone, msanii wa Kenya. Christina Shusho amekuwa rafiki yake kwa miaka mingi. Wakati aliposikia ringtone anataka kuacha mziki wa injili, alimtafuta ili aweze kuongea naye. Wawili hawa waliamua kufanya colabo kwa jina “tenda wema” yenye ilifanya vizuri sana.

Nyimbo za Christina Shusho.

 1. Napenda
 2. Unikumbuke
 3. Nipe Macho
 4. Akutendee nini
 5. Mtetezi wangu
 6. Hapo mwanzo
 7. Nitayainua macho
 8. Nataka nimuone Yesu
 9. Mshukuru bwana
 10. Wakuabudiwa
 11. Ushiriki na Roho
 12. Ebenezer
 13. Ongeza hatua zangu
 14. Yote alimaliza
 15. Tenda wema nenda zako
 16. Mapito
 17. Nataka nikae
 18. Mungu Uhimidiwe
 19. Bado nakungoja
 20. Territory
 21. Pendo la Mungu
 22. U mwema wakati wote
 23. Mungu wa huruma
 24. Hallelujah
 25. Unaweza
 26. Songa mbele
 27. All I need
 28. I’m gonna
 29. Wastahili
 30. All I need
 31. Nina wimbo
 32. Bwana utetenao

Shusho alisema hawezi ku perform kwa mikutano ya siasa kwani haileti picha nzuri kwa mashabiki wake na pia hairuhusiwi pia kwa mkristo ila hana tatizo nyimbo zake zikichezwa kwa mikutano ya siasa.

Bali na mziki, Christina Shusho ni mfanyi biashara. Ni mmiliki wa modeling agency nchini Tanzania. Kulingana na yeye haimanishi kama umeokoka usivae vizuri kama wengi wanavyodhania. Unafaa kuwa smart Ila nguo ziwe za heshima.

Christina Shusho aliokoka akiwa na umri wa miaka kumi na tano. Kama nilivyotangulia kusema amelelewa kwa maisha ya ukristo na mda mwingi alikuwa yumo kanisani. Ameolewa na John ambaye ni pastor. Bwanake Shusho amekuwa akimpa sapoti Shusho. Wako na watoto watatu, wasichana wawili na mvulana mmoja. Majina yao ni Hope Shusho, Odesia Shusho na George Shusho.

Kuna mda ilisemekana kuwa Christina Shusho wameachana na mumewe Ila baadae iligunduliwa kuwa haikuwa kweli

Soma hii ( historia ya nyota Ndogo)

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *