MaishaSanaa

Historia ya Nyota Ndogo

Nyota ndogo ni msanii amekuwa akigonga vichwa vya habari kwani kila kukicha Kuna jipya. Sio wengi wanaelewa vizuri historia ya Nyota ndogo kwani ni msanii aliyepitia mengi kabla ya kufika hapo alipo.

Kwa ufupi, Nyota ndogo ni mama wa watoto wawili, mvulana na msichana. Ako kwenye ndoa na mume wake mzungu kwa jina Nelson. Mengi yameongelewa kuhusu msanii huyu wengi wakisema alitafuta mzungu ili afaidi hela zake.

Nyota Ndogo wedding photos

Nyota ndogo amekuwa akijitetea kwani yeye anasema kuwa hamtegemei kabisa mzungu wake. Kulingana na Nyota ndogo, mzungu alimpata tayari akiwa na hela kwani anamiliki nyumba kadhaa za kukodisha na pia ana biashara Mbali mbali ikiwemo hoteli na bodaboda.

Kulikuwa na tetesi kwamba mzungu wake amemuacha na Nyota ndogo amekuwa akifanya juu chini ili kurudiana naye. Kwa sasa mambo yanaonekana kuenda sawa kwani Nyota ndogo Ali share screenshot ya chat akionyesha vile bwanake amemkosa.

Nyota Ndogo children

Msanii Nyota ndogo ni mzaliwa wa Pwani ya kenya mjini Mombasa. Nyota ndogo hakuweza kuyamaliza masomo yake kwa sababu ya ukosefu wa Karo na hapo ndipo akaamua kuwa mfanyi Kazi za nyumbani ( house maid)

Babake Abdul Abdala Atib alikuwa pia mwanamziki tajika sana na alikuwa mmoja wa bedi moja mjini Mombasa. Wasanii waliomfanya Nyota ndogo kupenda mziki ni kikosi Cha K – South. Alitamani sana kuwa mwanamziki na hapo ndipo Marehemu Andrew Burchell, mtayarishaji wa mziki kutoka nchi za ulaya alipogundua kipaji Cha Nyota ndogo. Kwa wakati huo, Andrew Burchell alikuwa anaishi nchini kenya.

historia ya nyota Ndogo

Kati ya zile album alizoachia Nyota ndogo ni pamoja na Chereko, Nimetoka Mbali, mpenzi na mama wakambo. Aliwahi kushinda tuzo za Kisima Awards mwaka wa 2003 kama mwanamziki bora wa Taarab na mwaka wa 2005 akashinda tuzo nyengine ya mwanamziki bora wa kike.

Hakukomea hapo kwani nyimbo yake tajika watu na viatu iliwahi kuchaguliwa kuwania tuzo za PAM awards mwaka wa 2007 na pia tuzo za Tanzania music awards kama nyimbo bora afrika mashariki.

Nyota Ndogo age

Nyimbo yake ” Take care” iliwahi kuwa kwa international world 2003 compilation album nayo “Chereko ikawa kwenye Rough Guide ya album ya Music of Kenya compilation.

Aliwahi kufanya colabo na wasanii kadhaa akiwemo Nonini nyimbo ya Nibebe, Necessary Noize ” Nataka toa”. Wasanii wengine aliyefanya nao colabo ni pamoja na Mr. Blue, Ally B na Q Chilla. Colabo hizi zilichangia pakubwa kwa safari ya mziki wake kwani alichaguliwa kuwania tuzo za Kilimanjaro awards.

Colabo za Nyota hazikukomea hapo kwani yeye chege Tmk na bobby mapesa walifanya nyimbo pamoja kwa jina ” Nawachanganya” chini ya producer Shirko.

Nyota ndogo amekuwa akiwakilisha Kenya kwa tamasha mbalimbali barani afrika ikiwemo sauti ya busara na Ziff ndani ya Zanzibar. Nchi zingine amewakilisha nchi ya Kenya ni pamoja na comoros, Dubai, Germany pamoja na south africa.

Nyota ndogo aliwahi kufanya Kazi kama mtangazaji wa Baraka FM iliyoko mombasa. Mwaka wa 2003 alikuwa mmoja wa judge ndani ya show kubwa inayofahamika kama tusker project fame. Mwaka huo huo alishinda tuzo ya Best coast female artist. Nyimbo yake iliyotetemesha afrika mpaka wa leo ni ” watu na viatu” nyimbo hii ilimuingizia hela ndefu sana kwani ilimpa show afrika nzima.

Nyimbo nyengine ya Nyota ndogo inayofanya vizuri ni ” je wewe’ ambayo ipo kwa youtube. Inapata mapokezi mazuri ndani ya radio na television.

Kwa mengi zaidi kuhusiana na mziki wa nyota Ndogo, unaweza ukatembelea YouTube channel yake ili uweze kuzipata nyimbo zake zikiwemo mpya na za zamani kidogo kama vile watu na viatu na nyimbo zinginezo. Nyota Ndogo pia hufanya na live band na kama unaweza kuwa na tamasha ya Aina yoyote basi unaweza wasiliana naye kupitia email Facebook account yake ” Nyota Ndogo” 

Asanteni sana kwa kufuatilia habari zetu hapa mwangaza news. Ili usipitwe na lolote, bonyeza kengele nyekundu iliyoko pembeni ndio kila siku uwe wa kwanza kuzipata habari zetu.

Soma hii pia : Makena Njeri atangaza rasmi kuwa yeye ni Gay

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *