InternationalMaisha

Makena Njeri atangaza rasmi kuwa yeye ni Gay

Kwa majina kamili naitwa Chris Makena Njeri. Nina furaha na siogopi kitu chochote” ndivyo alivyosema katika mahojiano ya Ted Talk aliyekuwa mwanahabari wa kituo Cha BBC, Makena Njeri.

Video ya Makena Njeri imekuwa ikigonga vyombo vya habari kwa mda sasa. Kumbuka Ted Talk ni kituo kinachojulikana ulimwengu mzima.

Makena Njeri atangaza rasmi kuwa yeye ni Gay

Makena Njeri ambaye anaishi Nairobi Kenya alijitokeza waziwazi na kusema yeye ni Gay. Kwa mda sasa, Makena Njeri amekuwa akisemekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Michelle Ntalami amabye ni C.E.O wa kampuni ya Marini Natural japo alikuwa akidai kuwa Michelle Ntalami ni rafiki tu kama wale wengine.

Makena Njeri ambaye alikuwa muigizaji wa mchezo ya Tahidi high amekuwa akihusika kwa kutetea uhusiano wa jinsia moja. Kuna wakati gari yake iliwahi kuharibiwa na mwanamke aliyedai kuwa Makena Njeri anamchezea kimapenzi. Japo hakuwa kwenye hilo tukio, Makena Njeri alipata simu nyingi kutoka kwa familia na marafiki waliomuelezea kuhusiana na mwanamke huyo.

Makena Njeri ex girlfriend

” Nakumbuka mwaka wa 2019 mwezi wa July asubuhi nilipoamka na kuangalia simu yangu nilipata meseji zaidi ya 1000 na missed call mia tano. Niliogopa sana kwani nilijua lazima Kuna kitu kibaya” alisema Makena Njeri.

Baada ya tukio hilo, mwanadada huyu anasema alipitia wakati mgumu kwa mda wa miezi mitatu mpaka akapoteza marafiki wake wengi. Kuna wanafamilia wake walimtenga na hata kujidai hawamfahamu kabisa. Makena Njeri ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu aliongezea kusema kwamba Kuna Kazi ya filamu alipewa Ila akakataa kuifanya kwani haikuwa inazingatia jinsia yake inavyopaswa.

Makena Njeri alisema alichagua kufanya Kazi inayofanywa na wanaume ambapo wenye Kazi walianza kumkejeli na kumcheka wakishang’aa yeye kama mwanamke ataweza aje kufanya Kazi ya wanaume.

” Nakumbuka kwa Mara ya kwanza katika maisha yangu nilijiangalia kwa kioo na nikasema, “Mimi ni shoga”, nipo tofauti na huo ndio ukweli.. saa hii najihisi nipo huru….”

Makena Njeri aliacha Kazi BBC na kwa sasa anafanya Kazi na Bold Network Africa chama kinachofundisha watu kuhusiana na LGBTQ kupitia filamu na documentaries.

Soma hii pia ( historia ya Ryan Mwenda wa Zora Citizen Tv)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *