AfyaMaisha

FAHAMU TATIZO LA KUUMWA NA TUMBO

FAHAMU TATIZO LA KUUMWA NA TUMBO; Ni watu wengi sana wanaosumbuliwa na tatizo hili la kuumwa na tumbo. Hii sio lazima uwe na umri flani eti uwe mzee ama mtoto. Maumivu ya tumbo inaweza Kuta kila mtu bila kuzingatia umri wake.

Kuumwa na tumbo husababishwa na sababu mbalimbali. Sababu hizi tofauti huleta maumivu ya tumbo. Wakati mwingi haya maumivu sio mengi ama ya kutisha kwani yaweza tibiwa na yakapona

Mara zingine maumivu haya huenda ikaweka maisha yako kwenye hatari. Haya maumivu huwa ni tofauti kwa kila binadamu na pia huenda ukaumwa na tumbo nzima ama upande mmoja wa tumbo.

Sababu zinazochangia maumivu ya tumbo.

Zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo. Kila chanzo Cha maumivu inategemea hayo maumivu yanatoka upande gani.

Kama unahisi maumivu chini ya upande wa kulia wa mbavu huenda imeletwa na;

  • (Kidney stones) Mawe kwenye mfuko wa nyongo
  • (Cholecystitis) maambukizi mwenye mfuko wa nyongo
  • Ini kuvimba
  • Jipu kwenye ini
  • Homa kwenye ini
  • Saratani ya kifuko Cha nyongo ( kongosho)

Kama unahisi maumivu chini ya chembe cha Moyo basi sababu itakuwa

  • Vidonda kwenye tumbo
  • Kiungulia
  • Cancer ya tumbo
  • Cancer ya kongosho

Kama maumivu inatoka pembeni mwa kitovu basi itakuwa ni

  • Kidney stones ama mawe ya figo
  • Maambukizi kwenye figo ama kwa kimombo ( pyelonephritis)
  • Acute appendicitis ama maambukizi ya kidole tumbo

Kama maumivu inatoka chini ya kitovu

  1. Maambukizi kwenye mfuko wa mkojo
  2. Klamidia ambao ni ugonjwa wa zinaa
  3. Uvimbe kwenye uzazi
  4. Uharibikaji wa mimba
  5. Saratani ya kibofu Cha mkojo
  6. Premenstrual syndrome
  7. Maumivu chini ya kitovu

Sababu zinginezo za kuumwa na tumbo ni;

  • Irritable bowel syndrome
  • Intestinal obstruction ama kujiziba kwa utumbo
  • Kujisokota kwa utumbo
  • Food poisoning
  • Kuwa na allergy ya chakula
  • Hernia ama ngiri

Typhoid fever ama homa ya tumbo

Ili Kutibu maumivu ya tumbo, ni lazima ujue sababu iliyochangia kuumwa na tumbo. Wakati ukingojea matibabu hospitalini, unaweza tumia dawa kama paracetamol ama Diclofenac ili kupunguza maumivu japo sio vizuri kutumia dawa za maumivu kutuliza tumbo Mara kwa mara. Kitu Cha kwanza kabla daktari hajakupa matibabu, mwanzo atafanya uchunguzi ili kuelewa historia ya maumivu yako

Baada ya uchunguzi wa daktari hapo ndipo atakapoamua matibabu aidha atakuchoma sindano, tembe ama upasuaji. Ni vizuri kula chakula bora na kutumiwa food supplements ili kuwa na afya nzuri.

Soma hii pia: njia za kupunguza uzito

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *