Maisha

Historia ya Alikiba

Ali kiba ni mwanamziki kutoka nchi ya Tanzania. Ni mwandishi wa nyimbo anayeheshimika sana. Alikiba alizaliwa November tarehe 26 mwaka wa 1986.

Alikiba photos

Alikiba ni Kati ya wasanii wanapendwa sana nchini Tanzania na africa mashariki kwa jumla. Ni hivi majuzi alifunga pingu za maisha na mchumba wake wa mda mrefu Amina Khalef ambaye ni mwanamke mrembo zaidi kutokea nchi ya Kenya. Kwa sasa Alikiba na Amina Khalef wako na watoto wawili.

alikiba children's

Alikiba sio msanii mdogo kama wengi wanavyofikiria. Kwa sasa anajulikana ulimwengu mzima na nyimbo zake zinachezwa karibia nchi zote duniani. Kumbuka msanii huyu ako na mkataba na Sony music, kampuni inayojulikana sana duniani.

Alikiba wife

Wakati wa jakaya Mrisho Kikwete, Alikiba alitabuliwa na rais kikwete kwa mchango wake mkubwa katika sanaa. Kwa sasa ana wafuasi duniani nzima na kila nchi anakubalika kwa burudani yake ya kukata na shoka. Alikiba alisomea shule ya msingi ya Upanga iliyoko Dar es salaam na baadae kuendelea na masomo ya shule ya upili.

Alikiba kids

Akiwa shuleni, Alikiba alipenda sana mziki na pia kucheza akiwa na marafiki zake. Pia alikuwa katika kikundi cha drama. Mwaka wa 2004, Alikiba alianza rasmi mziki na hapo ndipo aliporekodi nyimbo yake ya kwanza kwa jina Maria. Hii nyimbo ilipendwa sana nchini Tanzania.

mke wa Alikiba

Mwaka wa 2005, msanii huyu alialikwa kujiunga na team ya mpira nchini Uganda Ila akalikataa ombi hilo kwani alitaka kuendelea na mziki.

Soma hii : njia za kupunguza uzito

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *