MaishaSanaa

Nyota ya Ryan Mwenda Zora yazidi kung’aa

Ryan Mwenda ni muigizaji mkuu ndani ya tamthilia ya Zora inayopeperushwa citizen Tv kila siku ya wiki. Anaigiza kama “Simba” ni kakake muigizaji mkuu wa kike Zora ambaye jina lake kamili ni Sarah Hassan.

ryan mwenda tribe

Katika tamthilia ya Zora, Ryan Mwenda ni mvulana anayeonekana kusumbua na Yuko tayari kumtetea mamake kwa njia yoyote ile kwa yeyote yule anayemchezea kimapenzi ama kwa njia yoyote ile.

 

Muigizaji huyu anapendwa na watazamaji wengi wa Zora kwani yeye anaonekana kuwa jasiri na kusema kweli anajua kuigiza.

Ryan Mwenda ambaye kwa sasa ana umri wa miaka kumi na tatu hakujulikana leo kwani jina lake linafahamika hata kabla ya kujiunga na Zora. Amekuwa kwa sanaa tangu akiwa mdogo kwani hata ashawahi kuigiza ndani ya churchill show.

ryan mwenda photos

 

Mwaka wa 2016, Ryan Mwenda aliwahi kuhutubia wanachama wa jubilee huku aliwaomba wanainchi wote waweze kumchagua Uhuru kenyatta na naibu wa rais william Ruto kwa Mara ya pili.

ryan mwenda class

Hii ilimfanya rais Uhuru kenyatta kumpenda zaidi. Aliwahi alipiga picha na rais Uhuru kenyatta na picha hiyo ilisambaa mitandao. Akiongea mbele ya rais, Ryan Mwenda alimhakikishia rais Uhuru kenyatta kwamba atashinda uchaguzi mwaka wa 2017 na ikawa hivo.

Kutoka siku hiyo, Ryan Mwenda amekuwa akikutana na watu mashuhuri sana wakiwemo waziri wa usalama Fred Matiang’i, aliyekuwa gavana wa Nairobi bwana mike mbuvi sonko na seneta wa Nairobi bwana Johnson Sakaja.

ryan mwenda phone number

Ryan Mwenda amekuwa akiwahimiza wakenya wajichunge kutokana na adhari za virusi vya covid na wasifikirie serikali haifanyi bidii kwa swala nzima la covid 19 kwani janga la corona ni la kimataifa.

“Watoi wenzangu, season ya kuride bike si saahii. Rieng ni kusoma, kumanga na kutulia kwa keja”

Mwaka wa 2020 alijiunga na wanainchi wengine kwenye kampeni ya kuosha mikono,kuvaa barakoa na swala nzima la social distance kama njia ya kuizuia maambukizi ya covid-19. Ryan Mwenda ni mwanafunzi katika shule ya Riara springs Academy. Anapenda sana kucheza mpira mda wake wa ziada.

Soma hii pia : Waigizaji wa Zora na majina yao kamili

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *