Zora Citizen Tv : Waigizaji wa Zora Citizen Tv
Zora Citizen Tv
Ni tamthilia mpya ndani ya citizen Tv. Hii ni baada ya kipindi tajika Cha Maria kufika kikomo. Zora imetayarishwa na Lulu Hassan ambaye pia ndiye alikuwa mtayarishaji mkuu wa tamthilia ya maria.
Zora citizen Tv inasemekana kuwa ya gharama ya juu kwani kumetumika chopper na magari ya kifahari.
Waigizaji wa Zora Citizen Tv
- Jackie mutubia
- Sarah Hassan
- Salome sulubu
- Bridget Shighadi
- Blessing Lungaho
- Neema Sulubu
- Quincy Ando
- Robert Agengo
- Ryan Mwenda

Ryan Mwenda ana umri mdogo ila jina lake kwa sasa lipo juu kwani wakenya wengi wanamfahamu. Akiwa bado mdogo aliweza kukutana na watu mashuhuri kama vile rais Uhuru kenyatta, naibu wa rais william Ruto, Hon. Mike sonko na Daniel Ndambuki mwenye amechangia sana kukuza talanta yake.
Akiwa na kama miaka nane, Ryan Mwenda alijitokeza ndani ya churchill show kama mchekeshaji na akawa mchekeshaji mdogo nchini kenya. Talanta yake imempeleka mbali kwani saa hii ni muigizaji ndani ya tamthilia ya zora inayopeperushwa ndani ya citizen Tv.
Soma hii pia ( Waigizaji wa Pete maisha magic)