Uhuru kenyatta ahudhuria mazishi ya Magufuli
Rais Uhuru kenyatta amewasili Dodoma siku ya leo asubuhi kumuaga rais mwenzake wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.
Rais kenyatta ni mwenyekiti wa East African community ambapo Tanzania pia wako kwa huo muungano. Rais Uhuru kenyatta amemsifia magufuli kwa Kazi nzuri aliyoifanya.
” Afrika imempoteza kiongozi jasiri mwenye maono mazuri kwa nchi yake ya Tanzania. Sio Tanzania tu ila pia nchi zote ziliopo East africa community. Nimempoteza rafiki yangu na mwenzangu”
Viongozi wengine waliohudhuria mazishi ya magufuli ni pamoja na Cyril Ramaphosa kutoka afrika kusini, Felix Tshisekedi ( Dr Congo president), Emmerson Mnangagwa (Zimbabwe President); Edouard Ngirente (waziri mkuu wa Rwanda); Filipe Nyusi(Rais wa Mozambique ); Lazarus Chakwera (Rais wa Malawi) and Edgar Chagwa Lungu (Rais wa Zambia).
Magufuli aliaga dunia tarehe kumi na nane mwezi wa tatu 2021 baada ya kuugua ugonjwa wa moyo katika hospitali ya Mzena iliyoko dar es salaam.

Kabla ya kifo chake, magufuli alitoweka kwa uma kwa mda wa wiki moja ambapo taarifa za hapa na pale zilitapakaa kite duniani kuwa anaumwa. Siku ya mwisho Magufuli kupatikana hadharani ilikuwa February 27. Kutoweka kwake kuliibua maswali mengi huku wapinzani wake na wanainchi wakitaka kujua alipokuwa.
Kwa sasa Tanzania yaomboleza kwa siku ishirini na moja kwa kumpoteza rais wao wa tano huku Kenya pia ikijiunga na majirani Tanzania kwa maombolezi kwa kupeperusha bendera nusu mlingoti kwa siku saba.
Uganda pia hawajaachwa nyuma kwani pia wanaomboleza kwa siku kumi na nne na bendera pia nchini humo zitapeperushwa nusu mlingoti kwa mda wa siku kumi na nne.

Samia suluhu Hassan aliapishwa kama rais wa muungano wa jamahuri ya Tanzania baada ya kifo Cha magufuli. Lala salama dr magufuli hakika tutakukumbuka daima.