Maisha

Historia ya Kihenjo Kameme FM

Historia ya Kihenjo Kameme FM, Kihenjo lishakuwa jina la familia sasa. Kihenjo ni mtangazaji wa Radio ya Kameme FM nchini kenya ambapo kwenye radion hujuita Kizangala. Majina yake kamili Anajulikana kama Joel Mungai. Kihenjo anatamgaza kwa show almaarufu kama Cajamuka wakiwa pamoja na Muthoni Kirumba ambaye pia ni mtangazaji matata sana.

Kihenjo Kameme FM

Wengi wanamjua kihenjo kama mchekeshaji wa sinema za kikuyu sanasana wanaoelewa lugha ya kikuyu. Ako na show yake ndani ya Kameme Fm ya vichekesho anayoiendesha kila siku saa moja na nusu usiku.

Kulingana na utafiti wetu, mzee kihenjo amekuwa kwa Sanaa ya vichekesho miaka zaidi ya 25. Kwa wale wakikuyu walimjua miaka ya hapo nyuma watakubaliana na Mimi kwamba kihenjo alikuwa maarufu sana hata kabla hajaanza Kazi ya utangazaji kwenye radio.

wife kihenjo family

Wakati huo alikuwa akiigiza kama mzee huku amevalia mavazi ya kuraruka. Wengi walidhania yeye ni mzee kwani hata ndevu zake alikuwa akizipaka rangi nyeupe kuashiria uzee huku akitumia mkongojo (walking stick). Alikuwa akitengeza hela ndefu kwani alikuwa akiuza CD’s za Kazi zake za ucheshi. Pia alifanya Kazi za mcee kwa sherehe tofauti hadi kanisani japo sio zote zilimlipa.

Kihenjo ni Kati ya wale watu wenye hawapendi kutangaza maisha yao ya ndani. Sio Mara nyingi utapata kihenjo akiongelea familia yake kama vile mke na watoto. Hata mda mwingi akiwa radioni utamsikia akimtaja “Majangwa” ambaye sio mke wake halali Ila mke wake wa kuigiza naye.

Soma hii pia : maisha ya Muthoni wa Kirumba

Soma hii pia: historia ya Christina Shusho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *