InternationalMchipuko

Historia ya mtume Muhammad

Kwa wale wamekuwa wakiulizia mengi kuhusu Historia ya mtume Muhammad, chukua kiti na ukae sehemu tulivu ili niweze kukupasha mengi kuhusiana na mtume muhammad.

Kuzaliwa kwa Muhammad na maisha yake ya utotoni

Muhammad alipitia maisha magumu ya utotoni kwani alijipata yatima alipozaliwa kwani Babake aliaga duniani kabla ya kuzaliwa kwake.

Haikuishia hapo kwani alipozaliwa alikuwa na mda mfupi kuishi na mamake Amina aliyefariki muhammad akiwa bado mdogo. Wakati mamake anaaga dunia, muhammad alikuwa na umri wa miaka sita.

Baada ya kuwapoteza wazazi wake wawili na kuwa yatima, muhammad alichukuliwa na Babu yake na kuenda kuishi naye. Kwa bahati mbaya, muhammad hakuishi mda mrefu na Babu yake kwani babu yake pia alifariki baada ya miaka miwili.

Ilibidi ami yake Abu Talib aichukue jukumu la kumlea. Abu talib aliishi na muhammad mpaka akafikia umri wa kuoa. Abu talib alijitweka jukumu la kumuoza muhammad na kumpa himaya ambapo wakati huu muhammad alikuwa ashaanza Kazi yake ya kueneza ujumbe wa mwenyezi Mungu kwa watu.

Kulingana na hadithi za kiislamu, makuhani wa kiyahudi na mitume, mapadri wa kinasara, wenyeji wa bara la kiarabu walikuwa wakieneza neno kwa majirani kuhusu kuja kwa mtume. Wengi wa majirani hawa walikuwa wanaabudu sanamu. Wengi wa makuhani hawa waliwaonya majirani wao kwa ibada zao mbovu huku wakiwahikishishia kwamba mtume Muhammad atakapokuja atabadilisha ibada zao zote.

Waarabu walipoambiwa hivo walitaka kujua jina la mtume huyo na walipolijua jina lake muhammad walifurahia sana. Wenye kusadiki maneno hayo waliamua kuwaita watoto wao waliozaliwa mda huo muhammad.

Sio idadi kubwa iliyokubali kuwaita watoto wao muhammad maana jina lilipoanza kushika ama kutangaza, ndani ya bara arabu hawakuwa wengi wenye jina hilo.

Tangu akiwa mdogo, mtume Muhammad alikuwa na akili ya kiutu uzima na ni mtoto aliyeonekana kuwa mkomavu hivo sifa alizipata tangu akiwa mtoto. Akiwa mdogo hakupitia maisha kama ya watoto wengine kama kuchezea vitu vya kitoto. Inasemekana kwake alitaka kufanya vitendo vya kitoto Mara mbili tu ila naye Mungu akamhifadhi.

Kati ya vitendo hivo, mojawapo ni kwamba alitaka kwenda  kwa harusi ya marafiki wake waliooana mjini makka. Cha ajabu Mungu alimpa usingizi mzito sana siku hizo za harusi za marafiki zake mpaka hakuweza kutoka kwenda popote.

Mtume Muhammad hakuwahi kwenda kwa tamasha yote yenye kuabudu sanamu ama hata kula chakula chochote kile kilichotayarishwa kwa ajili ya sherehe za ibada za sanamu. Moyo wake hakuwahi kupenda ibada yoyote iliyohusiana na ibada za sanamu.

Katika maisha yake akiwa mdogo, mtume hakuwahi kuwa na sifa yoyote mbaya. Kulingana na watu wa umri wake wakati huo, hakuna hata mmoja aliyekuwa na sifa nzuri kama zake. Sifa zake ni zile sifa zinazosemekana kuwa sifa bora zaidi katika maisha ya kiislamu.

Kuna siku moja mkewe Aisha alipoulizwa ataje sifa za muhammad naye akawa mwepesi wa maneno na kusema, sifa za muhammad ni zile zilizotajwa na kusifiwa na Quran ambapo zipo chungu nzima.

Mtume Muhammad alikuwa hayafichi matendo mabaya ya makafiri. Muhammad alijuvunia na kusema hakuwahi kuyafanya matendo kama vile kuabudu sanamu, kulewa, kuzini, kucheza kamari wala kumuibia ama kumdulumu yeyote yule kitu chake.

Wakaazi wa makka walikuwa wakimsifia sana mtume Muhammad kwani alikuwa mtiifu, mwaminifu, mpole na mwenye sifa zaidi. Sifa zake zilichangia mpaka wakaazi wa makka wakampa majina zaidi na kumuita muhammad Al-Amin (mwaminifu). Heshima ilizidi kwani wengi wakubwa kwa wadogo walikuwa wanampa amana zao awawekee.

Wake wa Muhammad

Kama mjuavyo, quran inaruhusu wake wanne. Kwake muhammad ilikuwa tofauti kwani yeye alisema anaruhusiwa kuvuka kiwango hicho na kuongeza wake wengine. Muhammad alioa wanawake kumi na moja majina yao yakiwa kama yafuatayo.

Khadija binti khuwaylid

Khadija aliolewa mwaka wa 595 na kuaga dunia mwaka wa 620 mwezi wa January. Khadija alizaa mabinti wanne na muhammad. Mabinti Hawa ni; Ruqayya, Umm Khulthûm, Zaynab na Fatima. Pia walipata watoto wawili wa kiume wakiwemo Qàsim na And Allah ila walikufa wakiwa bado wadogo.

Sawda binti Sam’a

Sawda aliolewa mwezi wa March mwaka wa 620

Aysha Binti Abu Bark

Aysha naye aliolewa mwaka wa 623 akiwa na umri wa miaka tisa

Hafsa binti Umar.

Huyu aliolewa mwaka wa 624 mwezi wa novemba

Zaynab Binti khuzayma

Kuolewa kwake ni tangu juni mwaka wa 625. Alipatana na mauti yake agosti mwaka 625.

Hindi umm Salama Binti Andi umayya

Aliolewa February 625. Aliwahi kuolewa na mwanaume mmoja na kuachiwa watoto wengi. Pia alikuwa mtoto wa kambo wa shangaziye mohamed.

Zaynab Binti jahsh.

Kaolewa June mwaka wa 626. Alikuwa binamu yake mohamed Aliachwa na mume wake.

Juwayriya Binti Al Harith

Aliolewa tangu December 626

Ramla Umm Habība binti Abi Sufyan.

Aliolewa tangu August 628. Aliachana na mume wake aliengia ukristo.

Safiyya Binti Huyay

Aliolewa September mwaka wa 628. Kabla ya kuolewa alikuwa mmoja wa wayahudi waliotekwa nyara katika vita vya khybar.

Maymuna Binti Harith.

Huyu naye aliolewa February 629 akiwa na miaka hamsini na moja.

Kati ya wanawake hawa wote, ni mwanamke wa kwanza tu aliyepata watoto na mtume Muhammad. Cha kushangaza ni kwamba hawa watoto walifariki kabla ya baba yao isipokuwa Fatma aliyeaga miezi sita baada ya Babake kufariki.

bali na wake wa kihalali, Quran inakubalia kuwa na masuria wasio na idadi (dhāt al-yamīn, “waliomilikiwa na mkono wa kuume”, kwa jina nyengine wanafahamika kama watumwa, hasa wale wanaopatikana kwa kutekwa vitani). Mtume Muhammad alikuwa na kama hawa kumi na sita: Marya ambaye alikuwa Mkristo ni Kati ya hao watumwa na alimzalia mtoto wa kiume: Ibrahim, aliaga dunia akiwa bado mdogo sana. Baadaye Babake kwa Huzuni kubwa alimfuata mwanawe kaburini mda mfupi baada ya kifo chake.

Maisha ya Muhammad kabla ya kuwa mtume.

Kama kuna watu walitambulika kwa kupenda biashara ni makureshi. Ungepata karibia makureshi wote walipitia hii kazi ya biashara.

Kati ya hizo safari zao za kibiashara kuelekea Yaman, Babake mdogo wa pili bwana zubeyr alimuomba muhammad kama angeweza Kuungana nao katika safari yao.

Mtume hakusita kwani alikubali kabisa kuwa miungoni mwa wanasafari walioelekea Yaman. Walikaa Yaman siku tatu kisha wakarudi nyumbani. Wakati huo mtume alikuwa ni mtoto mwenye umri wa miaka tisa.

Mtume alipofikisha miaka kumi na mbili aliamua kurudi tena Yaman lakini kwa mda huo aliandamana na Babake mdogo mwingine ambaye kama nikivyosema hapo awali alijukikana kama Bwana Abu Talib. Katika hii safari walikuwa waende shamu ila baada ya kufika busra, mji uliokuwa kusini katika maeneo ya Shamu, walikutana na Bahyra ambaye alikuwa padri. Bahyra alikataa katakata muhammad asijaribu kusonga zaidi ya pale walimofika na babake mdogo Abu Talib. Sababu ya kumkatalia ni kuwa, huyu padri alipomtazama muhammad aligundua kuwa alikuwa na alama zote za mtume. Aliogopa kwamba mtume angenda shamu huenda angeuliwa na wayahudi. Padri huyu alimuomba Abu Talib kumregesha mtume Muhammad nyumbani ama kama itawezekana atafute mtu mwingine mwaminifu arudi naye ndio Abu Talib aweze kuendelea na safari yake ya biashara. Abu talib hakubishana na alikubali kumpeana Mtume Muhammad kwa mtu arudi naye na yeye akaendelea na biashara zake.

Padri huyu alikuwa mmoja wa wanachuo wa kinasara. Aliwahi kumbashiri mtume lakini hakuwahi kumwamini alipoanza Kazi yake ya utume. Cha kushangaza ni kwamba padri huyu alikuwa na mwanafunzi wake kwa jina Salman Al-Farsy ambaye baada ya kusiskia habari ya mtume, alisilimu na kueneza uisilamu.

Mtume Muhammad alipifikisha miaka kumi na tano alianza kufanya biashara za hapa na pale akishirikiana na Said Bin Yazid. Hii biashara yao ilifanyika miji iliyokuwa karibu na makka. Baada ya kufanya biashara kwa mda, said bin Yazid alisilimu Jambo ambalo lilimfurahisha sana muhammad. Muhammad alipendwa na wengi kwani alikuwa mwaminifu katika biashara yake.

mtume muhammad alizaliwa mwaka gani,

Maisha ya Muhammad ndani ya makka

Muhammad aliishi mjini makka kwa miaka 53. Miaka arubaine akiwa bado hajakuwa mtume na miaka kumi na tatu baada ya kuupokea utume. Kwa miaka kumi na tatu, mtume aliishi makka akiwa mtume wa Mungu. Kutokea utotoni mwake, mtume alipitia maisha magumu na kama nilipotangulia kusema, alizaliwa akiwa yatima tayari.

Pia kwa vile maisha ya familia yake yalikuwa chini, yeye alikuwa yuafanya kazi ya kufuga mifugo ya watu ili kujikimu kimaisha. Kazi ya kufuga wanyama aliifanya katika ujana wake wote japo alilipwa pesa kidogo sana kwa kazi hiyo. Kazi hii alifanya mpaka alipofikisha miaka ishirini na tano baada ya kupata kazi kwa Khadija, bibi mtukufu wa kikureshi ambaye baada ya mda, alimuoa kama bibi yake na kuzaa naye

Maisha ya mtume Muhammad baada ya kuhamia Madina na mwanzo wa Umma.

Baada ya mda, mtume Muhammad alipokea wito ama amri ya kuhamia mji wa Madina. Alipofika huko alipokelewa vizuri huku wengi wajitolea kumlinda kutokana na maadui wake.

wayahudi huko Madina hawakukubaliana na yeye kama vile walikubaliana na manabii wa bibilia. Mtume hakukata tamaa na hao wayahudi hawakumzuia kuendelea kuhubiri neno la kweli. Akiwa bado yuwahubiri aliamua kuandika hati ya agano iliyokubalika na wamadina wote. Na hapo ndio asili ama mwanzo wa Umma ambayo ni jamii ya waumini.

Baada ya kuishi Madina kwa miaka kumi, wengi walikubali kuingia kwa dini ya uisilamu. Kumbuka huko Madina kuna makabila mingi ya kiarabu na wote walikubali kuingia dini ya uisilamu kwa makundi makundi.

Ilipofika mwaka wa 630 muhammad aliamua kurudi Makka ambapo wakati huu alikuwa na nguvu zake. Alipofika makka, aliiteka Makka na kufanya bidii ya kuirudisha Kaaba ambayo huwa Kibla Cha waisilamu inayotumika na waisilamu wote duniani wakati wa sala na hija.

Soma hii pia ( utaratibu wa mazishi ya kiisilamu)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *