Maisha

Huddah Monroe aeleza hela anayopokea

Huddah Monroe ni mwanadada anayejikulikana sana. Ako katika orodha ya wale wadada wanaoijita “socialites” na ni mwanamke tajiri sana. Ni mwanadada mwenye haogopi yeyote na ako tayari kufanya chochote kwa ajili ya pesa. Huwa ako vinywani mwa watu kwa mazuri na mabaya ila hilo halimhusu.

Huddah Monroe in white

Aliwahi kuwa kwa bigbrother africa na huenda uwepo wake kwenye big brother kulimsaidia kujulikana zaidi kwani ana wafuasi wengi sana sanasana kwa instagram. Kujulikana kwake na wengi kumemsaidia pakubwa sana kwa biashara yake.

Huddah Monroe

Kwa sasa Huddah Monroe anauza zaidi vitu vyake vya urembo kwani jina lake tayari ni soko. Nchini kenya, mwanadada huyu anasemekana kufaulu zaidi kuliko yeyote kwa biashara ya urembo. Hivi karibuni amejiunga na “Only fans”. Only fans ni show inayosemekana kuwa ya watu wazima na mambo yenye watu wanaongelea pale sio yakusikizwa ama kutazamwa na watoto wadogo.

Watu wenye wamejiunga na “only fans” huongea bila kuficha na ndio maana watoto wadogo hawatakikani kutazama hii show. Show ya Only fans” iko kwenye mitandao na wote wanaochangia hulipwa kutokana na mafans wanaowatazama.

Huddah chilling

Sio lazima kuongelea mambo ya watu wazima kwenye hii show ya “Only fans”. Wengi pia hujiunga pale na hufundisha mambo kama vile ya mazoezi, Kuweka mwili sawa, Afya ama pia mambo ya kifamilia. Kuitazama hii show lazima ulipie “Pay-per-View” (PPV)

Huddah Monroe anasemekana kupokea zaidi ya $ 17,000 kila mwezi. Hii ni kama milioni 1.7 za kikenya. Akielezea kuhusu “Only fans”, Huddah Monroe alisema hii sio show ya p**n kama wengi wanavyofikiria ila ni show ya kubadilishana mawazo na kusaidiana hata kwenye biashara.

 

View this post on Instagram

 

#HuddahMonroe say she made 1.7M on #OnlyFans in just 1 month ??

A post shared by Nairobi Gossip Club (@nairobi_gossip_club) on

Soma hii pia ( Betty Kyalo aelezea aina ya mwanume anayetaka kuzaa naye)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *