Utajiri wa harmonize, miaka na mengi zaidi
Utajiri wa harmonize ulianza kujitokeza vizuri alipoiaga kampuni ya WCB. Sio kuwa hakuwa na nyumba na magari wakati huo ila alikuwa hajatangaza utajiri wake. Kwa sasa anaonekana kufanikiwa zaidi na ako na hela za kisawasawa.
Harmonize alizaliwa nchini Tanzania mwaka wa 1991, October tarehe tatu. Ni msanii anayejulikana sana ulimwengu mzima. Nyimbo zake ni Kama vile Bado, Aiyola, matatizo na zote hizi zimefikisha views zaidi ya milioni tano ndani ya YouTube.
Harmonize ana miaka 27 na inasemekana ni Kati ya wale wasanii tajiri barani Africa.
Kwa Sasa ako kwenye mahusiano ya kimapenzi japo bado hawajajaliwa kupata watoto.

Utajiri wa harmonize
Kulingana na utafiti wetu, utajiri wa harmonize ni Kati ya dola milioni moja mpaka dollars million tano.
Nyumba ya Harmonize
Kama unakumbuka vizuri wakati harmonize alipotoka WCB ilibidi aweze kulipa kampuni hiyo millioni mia tano za Tanzania. Ilibidi auze nyumba zake mbili ili aweze kulipa deni. Hii haimanishi siku hizi hana nyumba. Msanii huyu ana bonge la Nyumba.
“Nimelipa kiasi lakini mpaka hivi sasa bado nadaiwa na sijamalizia kulipa ila bado kiasi kidogo sana cha kumalizia hela hiyo,” Harmonize alisema wakati akihojiwa kwenye kipindi cha XXL kinachoruka Clouds FM.
Ukimhitaji Harmonize kwa show, itabidi uwe umejihami na dola elfu kumi za kimarekani. Hizo ni kama millioni ishiri na tatu za kitanzania. Mkewe Sarah anasemekana kuwa na hela zaidi hata kumliko Harmonize mwenyewe. Sarah anasemekana kutoka kenye familia inayojihushisha na madini.

Gari ya Harmonize
Harmonize ako na magari zaidi ya tano, Hela anayoingiza kwa mziki wake ni nyingi ndio maana siwezi shangaa akiwa na magari hayo yote. aliwahi kupewa zawadi ya gari na mkewe hapo mwanzoni

Soma hapa (wasanii tajiri Tanzania)