Mziki

Wasanii matajiri tanzania

Najua ni vigumu kuweza kuwatambua Wasanii matajiri tanzania kwa kuwaangalia tu maana wengi huvalia kipesa ila hawana hela yoyote. Tanzania msanii anaweza akaishi maisha ya kifahari ukadhania ana hela nyingi kumbe anaiga tu.

Wasanii matajiri tanzania sio wengi sana ila nitakupatia orodha fupi ya majina yao na niweze kukuelezea ni akina nani. Cha msingi ni kuwa nchini Tanzania kuna vipaji na ni nchi ina wamziki wengi wanaojulikana dunia Nzima. Kulingana na utafiti wetu, tumeweza kuorodhesha zaidi ya top 10 ya Wasanii matajiri 2020.

Diamond Platnumz ( Naseeb Abdul )

Diamond platnumz | Wasanii tajiri tanzania

Huyu ni msanii mwenye tunaweza sema ameifungulia sanaa ya bongo kwa nchi za kimataifa na wasanii wa tanzania wanajivunia uwepo wa Diamond Platnumz. Amefanya colabo zaidi ya kumi na wasanii wa kimataifa na wengi wao aliweza kuwalipa ili waweze kukubali kufanya naye kazi. Ikija na mambo na kumiliki jukwaa, bingwa huyu anafanya makamuzi ya hali ya juu.

Akiwa juu ya stage anahakikisha ile pesa umeotoa mfukoni mwako ni ya haki kwani buradani yake ni ya hali ya juu. Mwaka wa 2009  ndio aliweza kujulikana zaidi na kama unakumbuka nyimbo yake ya Kamwambie, basi utakuwa unamuelewa zaidi.

Kulingana na utafiti wetu, Diamond Platnumz ndiye msanii tajiri tanzania na sio hapo tu mbali afrika mzima. Msanii huyu hupiga show kila wiki na ukimhitaji itabidi uweze kumpatia zaidi ya dola elfu arobaini $40,000. Diamond Platnumz tunaweza sema ni msanii tajiri Tanzania kwani ndiye anayeifungua orodha ya wasanii tajiri Tanzania.

Ana magari ya kila aina na nyumba za kifahari. Usisahau pia anafanya matangazo kwa kampuni tofauti tofauti. Pia ana mashamba makubwa sana na maduka ya kila aina.

Harmonize

Wasanii matajiri tanzania

Ni msanii anayeonekana kuwa na bidii sana. Alipojitotoa kwa label ya WCB, wengi walidhania labda mziki wake utaenda chini ila haikuwa hivo. Kwa sasa anazidi kuachia mziki mzuri. Hivi majuzi aliweza kumsajili msanii mpya kwa jina Ibraah. Msanii huyu ako kwenye list ya Wasanii matajiri Tanzania 2020.

Msanii huyu anafanya vizuri na anaonekana kuwa tegemeo kwa label yake Harmonize.  Harmonize ana magari za kifahari zaidi ya tano, Nyumba za kifahari na zaidi ya hayo, ameoa mke anayesemekana kutoka kwenye familia yenye hela nyingi.

Alikiba

Alikiba | Wasanii matajiri tanzania

Ni msanii ambaye amemakinika sana. Nyimbo zake hupendwa sana. Yeye hulinganishwa na Diamond platnumz kwani wawili hao huonekana kuwa na ushindani mkubwa. Alikiba ashafanya show nyingi sana nchi za ulaya na kusema kweli mziki wake unapendwa na wengi. Kutokana na hilo ana hela zaidi. Alikiba pia ako kwenye orodha ya Wasanii matajiri tanzania na kama sitomtaja orodha yangu itakuwa haijakamilika. Kumbuka pia Alikiba ashawahi orodheshwa kama mmoja wa wasanii matajiri africa 2020

Professor Jay (Joseph Haule)

Wasanii matajiri tanzania
Professor Jay

Ukiongelea kuhusu Wasanii 10 matajiri Tanzania 2020, Basi huwezi ukamsahau professor Jay. Ni msanii mkongwe ila jina lake bado lipo palepale.

Alianza mziki mwaka wa 1990 na band yake ilikuwa  ikijulikana kama hard blasters. Yeye ndiye alianzisha mziki wa kizazi kipya na Band yake ilikuwa ya kwanza kuucheza mziki huu wa kizazi kipya.Utajiri wake umetokana na show nyingi alizozifanya katika nchi za kigeni.

Ana jumba la kifahari na magari zaidi ya mawili na pia yeye ni mfanyi biashara. Kwa sasa ni mbunge na hii pia inamuongezea hela nyingi sana.

 Lady Jay Dee ( Jidith Wambura)

Wasanii matajiri tanzania | Lady Jay Dee
Lady jay Dee

Alianza mziki mwaka wa 1990. Kwa sasa ni mwanamziki wa kike anayeheshimiwa sana afrika mashariki. Hivi sana hayuko sana kwenye mziki kwani anashughulikia biashara zake ila bado mziki anaufanya. Ni mmoja kati ya wale wasanii waliweza kupata kipato kikubwa sana wakati mziki wa kizazi kipya ulipoanza.

Ana bidii sana na labda hii ndio imechangia utajiri wake. Kama niliowataja hapo awali, Lady Jay Dee ana nyumba za kukodisha na pia anaishi kwa nyumba ya kifahari. Ana magari zaidi ya tano.

AY ( Yesaya Ambena)

AY | TANZANIA
AY

Alianza mziki mwaka wa 2000 na kikundi chake kilijulikana kama East Coast. wanakikundi waliachana na AY akaamua kufanya mziki kivyake. Hapo ndipo walipatana na rafiki yake Mwana FA, Hamisi Mwinjuma na kwa sasa wamekuwa marafiki zaidi ya miaka kumi.

AY hapendi kujionyesha na yeye hufanya mambo yake kisiri. Hii haimanishi kuwa hana hela ndefu. AY ni mmoja wa Wasanii matajiri tanzania. Pesa zake nyingi alizipata kupitia show za kimataifa. Pia mwanamziki huu ana magari ya kifahari, nyumba za kikweli bila kusahau kampuni yake ya nguo na maduka sehemu nyingi Tanzania.

Msanii huyu anamiliki kampuni ya unity entertainment company inayotengeneza vipindi vya T.V. Kama uliwahi kutazama Mikasi Ndani ya E. Africa T.V ujue hiyo ni kazi ya kampuni ya Yesaya Ambena (AY).

Vanessa Mdee

vanessa mdee na Jux
vanessa mdee na Jux

Wakati unapoongelea wasanii wa kike wa nchini Tanzania, Lazima umtaje Vanessa Mdee, Mbali na uwanamziki, Yeye ashakuwa mtangazaji ndani ya MTV base. Video zake ndani ya youtube zinapata utazamaji mkubwa kwani yeye hufikisha millioni kwa kila video.

Vanessa mdee kama wenzake ako na biashara zake na kwa sasa ako kwenye uhusiano na R0timi ambaye ni muigizaji wa tamthilia inayopendwa zaidi kwa jina “Power”. Hapo mwanzoni alikuwa kenye uhusiano na Jux ila naona kila mtu aliamua kufuata njia zake.

Soma hii pia (je zuchu alihusika na kuachana kwa tanasha na diamond)

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *