MchipukoSanaa

Zuchu : sikuhusika kabisa kuachana kwa tanasha na diamond platnumz

Zuhuru “Zuchu” ambaye ni mwanawe Khadija kopa amekanusha madai kuwa alichangia diamond platnumz kuachana na tanasha.

Kwa mda Sasa fununu zimekuwa zikienea kila pembe ya Tanzania huku ikidaiwa kuwa diamond platnumz na Zuchu Wana uhusiano wa kimapenzi. Yote haya yalichangiwa na jinsi anavyomshughulikia kimziki na mambo mengine kuliko msanii wowote wa wasafi records.

Akiongea na vyombo vya habari nchini Tanzania, Zuchu alionekana kushtushwa sana na maneno hayo. Alisema hahusiki kabisa na kuachana kwa tanasha na diamond. Aliongezea kuwa anaheshimu sana boss wake diamond na familia yake kwa jumla. Alisema uhusiano wake yeye na diamond platnumz ni kazi na Hamna lingine.

” Mama alinionya tayari kuwa katika ulimwengu wa Sanaa, wengi wataongea mengi, ya kweli na ya uongo. Aliniambia nifunge maskio kwani nukiwaskiza sitaweza kutimiza malengo yangu…kwa hivyo hii ni maneno ya watu tu Ila sijahusika chochote na uhusiano wa tanasha na diamond platnumz….”

Zuchu na Khadija kopa
Zuchu na mamake Khadija kopa

Zuchu aliongezea kuwa anaheshimu uhusiano wa kila mtu na sio kwa diamond platnumz tu ila kwa yeyote Yule ako kwa uhusiano. Kwa Sasa hayuko tayari kuwa kwa uhusiano wowote kwani anataka kuyatumiza malengo yake.

” Nilitamani sana nafasi hii niliyopata kwa boss wangu diamond platnumz ndio maana kwa Sasa sitaki kujieka kwa skedo yoyote ama kuwa chanzo Cha kuvunjika kwa uhusiano wa yeyote…. Hapa nimekuja kazi tu Ila hamna lingine…”

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *