Maisha

Swahili | Lugha ya kishwahili

Swahili ni lugha na pia hujulikana Kama kiswahili. Hii lugha ya wabantu. wengi wanaongea lugha hii Kama lugha ya mama ama lugha ya pili. Wengi wanaotumia lugha hii hupatikana pwani kwenye nchi kadhaa za afrika.

Sehemu hizi ni Kama vile visiwa vya lamu ya Kenya na sehemu karibia zote nchini Tanzania.

Swahili culture ndani ya zanzibar

Swahili ama lugha ya kiswahili pia hupatikana Congo na wengi nchini Congo huongea kiswahili. Hii Ina maana kuwa Kuna wabantu ndani ya nchi ya Congo.

Wale watu huongea Swahili Kama lugha ya mama hujulikana Kama waswahili. Hii haimanishi Kuna kabila la kishwahili Ila Ina maanisha watu wanaoongea lugha ya kiswahili.

Swahili ni lugha inayotumika sana Tanzania na ndio lugha ya kwanza katika nchi hiyo “national language” wanavyosema wazungu. Kenya pia lugha hii inatambulika na baada ya kizungu, lugha ya pili ni Swahili.

Tukingia ndani ya Congo kinshasha, kiswahili ni lugha katika zile lugha nne kuu. Lugha yao kuu ni kifaransa lakini kiswahili hutumika pia.

Uganda pia Kuna watu wanaoongea Swahili Ila sio wengi. Kiswahili kinafahamika nchini humo na hata wasanii wengine huimba nyimbo na lugha ya kiswahili.

Kiswahili ama Swahili ilitokea uarabuni na ni neno lipo kwa lugha ya kiarabu sawāḥilī linalomanisha coast (pwani). Swahili ilitokea wakati waarabu waliingia katika visiwa vya afrika mashariki kufanya biashara. Hiyo ilifanyika miaka mingi sana iliyopita. Vile ilikuwa ni vigumu kuelewana, lugha ya wabantu ilichanganyikana na ya waarabu hapo ndipo pakazaliwa kiswahili na kukawa na Swahili culture.

swahili miji ya kale

Katika 19th century, kiswahili kilianza kusambaa karibia nchi zote za Africa mpaka wajerumani waakanza kuitumia sehemu za Tanganyika. Hii ilifanyika wakati tanganyika ilipokuwa yatawaliwa na wajerumani kabla ya Tanzania kupata Uhuru.

Kiswahili kilianza kuvutia nchi jirani Kama vile Kenya na Uganda japo hapo mwanzo hawakukichukulia kwa uzito. Kwa Sasa hata mashuleni kiswahili hufundishwa sanasana Africa mashariki.

Ndani ya Swahili Kuna lugha ndogondogo zilizotokana na lugha ya kiswahili. Lugha hizo zipo katika nchi tofauti tofauti.

Kiunguja – Ni lugha inayotumika sana Zanzibar na sehemu zingine chache huko Tanzania.

Kimvita – lugha inayotumika Mombasa Kenya sanasana katikati ya pwani

Kiamu- inapatikana visiwa vya lamu na sehemu chache za pwani

soma hii pia ( Jinsi ya kujua mwanmke anakupenda )

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *