Afya

jinsi ya kujikinga na ukimwi

Wengi wanachukulia jambo hili kwa mzaha ila gonjwa hili laua. Nimekuandalia mengi kuhusu jinsi ya kujikinga na ukimwi

Sio njia nyingi zinazoleta ukimwi lakini zipo njia tunaeza zuia ili wewe na mwenzako msiambukizane maradhi ya ukimwi. Watafiti wengi wamefanya utafiti kwa mda na wanaelezea kwa kina ya jinsi ya kujikinga na ukimwi na ukifuata maagizo haya, Basi utaepukana na hili gonjwa sugu.

Kuambukizwa ukimwi hutokana na kufanya mapenzi bila kinga na mtu mwenye virusi. Pia kutumia sindano yenye imetumika na mtu mwenye virusi. Kwa ufupi ukimwi husambazwa na majimaji ya mwili wa binadamu mwenye  virusi. Majimaji haya ni Kama vile damu, maji ya kizazi ama maji yanayobeba mbegu za kizazi (semen) na hata maziwa ya mama.

jinsi ya kujikinga na ukimwi

Tumia mipira ( Condoms) wakati unapofanya mapenzi. Hii ni njia mwafaka sanasana Kama unayefanya mapenzi naye ana virusi ama nyote wawili hamjapimwa ili kujua hali zenu. Mipira huzuia zaidi ya asilimia tisini ya virusi vya ukwimi.

Usijidunge na sindano yenye imetumika. Mara nyingi wanaotumia dawa za kulevya kwa njia ya sindano, hawazingatii Hali ya afya. Wengi hutumia sindano moja bila kujua virusi vya ukimwi/HIV zinaweza patikana kwa mmoja wao. Hii ni hatari zaidi na wengi wanapata virusi vya ukimwi hata bila kujua.

jinsi ya kujidunga na ukimwi | kujidunga sindano

Ili kuzipata virusi vya ukimwi lazima Yale majimaji ya aliye na virusi kupata mwanya sana sana kwa ngozi iliyokatika ama iliyowazi. Njia za kizazi za mwanamke ama mwanamme zipo na hatari kubwa kwani huwa zipo wazi.
Mdomo pia ni kiungo chenye Kiko hatarini maana kipo wazi. Viungo nilizotaja Zina aina ya majimaji yanayojulikana Kama mucous membrane yenye hubeba virusi vya ukimwi.

Mama mwenye virusi vya ukimwi anaweza akamwambukiza mtoto wakati anapomzaa na pia anapomnyonyesha. Kama mama ana ukimwi, Kuna njia hutumika ili kumkinga mtoto kupata virusi. Mama Kama huyu pia haruhusiwi kumnyonyesha mtoto.

Huwezi kupata ukimwi kwa kumsalimia mtu, kumkumbatia, kutumia choo kimoja ama hata kutumia sahani ama vikombe alivyotumia mtu mwenye virusi.

Jinsi ya kuzuia kusambaza ukimwi

Njia ya kwanza ni kuhakikisha mmepimwa kabla ya kuwa kwa uhusiano wa kimapenzi. Hii itasaidia pakubwa mno kwani mkijua hali zenu mtatafuta njia mwafaka za kujikinga.

Njia ya pili ni kupunguza wapenzi. Unapokuwa na wapenzi wengi ni hatari kwani hujui kila mpenzi anatembea na Nani na anayetembea naye ana virusi
au la.

jinsi ya kujikinga na ukimwi | dawa za ukimwi

Unapopatikana na ukimwi haimanishi ndio mwisho wako. Kuna dawa zinazopatikana kila nchi za kuzuia makali ya virusi vya ukimwi. Ukitumia hizo dawa inavyostahili basi utaendelea kuishi maisha yako kama kawaida bila hofu yoyote.

Soma hii pia ( Jinsi ya kuongeza damu mwilini)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *