MaishaMchipuko

mapenzi | ishara 23 zinazoonyesha kuwa mwanamke anakupenda

Mapenzi wakati mwingine hujitokeza kwa urahisi sana lakini sio rahisi kupata uhakika Kama mapenzi yenu yatakaa kwa mda gani kwani lazima nyote wawili muwe na hisia za kimapenzi kwa kiwango kikubwa.

Je,unadhani mpenzi wako uliye naye anakupenda,? Sio vigumu kuthibitisha haya kwani nimekuandalia ishara ishirini na tatu zakuonyesha kama mpenzi wako anakupenda au la.

Kumpenda mtu kwa dhati ni Jambo fiche sana kwani ni vigumu kuelewa chenye wafanya Kama mpenzi wako anapenda au la. Unaweza dhania chenye wafanyia mpenzi wako kinamfurahisha kumbe anavumilia tu.

Ikija kwa mapenzi, wanawake wanaonekana wenye Siri zaidi. Huwachukua mda wanawake kuongea wazi kuhusiana na hisia zao. Ukitazama ishara zao unaweza ukawasoma na huenda ukajua Kama Wana mapenzi au la.

Cha ajabu ni kuwa, wanawake wanapotoa ishara, wanategemea wanaume wawaelewe na wajue wanachomanisha. Mwanamke akikupenda, itakuwa vigumu kwake kuwa wazi kwako Ila atakuonyesha kwa ishara.

Sio wanaume wengi wanaelewa ishara hizi na wanaume wengi huogopa hata kuwaongelesha kuhusu mapenzi maana hawajui majibu watakayoyapata. Kulingana na utafiti wetu, ukiona wawili wakiogopona kuhusiana na maswala ya mapenzi inaashiria kuwa Kuna chemichemi za mapenzi Kati yao.

Ili kuwa kwa uhusiano mzuri na mwanamke, lazima ulewe mienendo yake, ishara anazozitoa kwako na mengineo nitakayoyataja. Ukifaulu haya yote, basi uko vizuri na unaweza kuwa na uhusiano hata wa mbali na mapenzi yenu yatafanikiwa.

1. Anaonyesha ishara za wivu

Mwanamke anayekupenda huonyeshwa ishara za wivu. Hapendi kukuona ukiongea na mwanamke yeyote. Wakati mwingine huenda akasirika hata ukiongea na msichana wa familia yako. Wakati mwingine hudhania labda unayeongea naye mko na uhusiano wa kimapenzi.

2. Hukuangalia machoni bila kuogopa

Ishara ya kwanza kabisa ni wakati mnapoangaliana macho kwa macho. Anapokuangalia machoni anaonyesha kuwa anakuamini na haogopi kuwa kwenye uhusiano na wewe.

3. Huonekana na wasiwasi anapokuona

Hii hujitokeza sana kwa wanawake wengi. Mnapokutana, anaonekana kutaka kujua utawaambia Nini. Wanachotegemea toka kwako ni maneno matamu ya kimahaba na bila shaka upo ndani ya Moyo wao.

4. Ishara ya sehemu mdomo kutetema

Ushawahi kumuona akitetemeka wakati anapokuongelesha, ishara za mwili huongea mengi sana na huonyeshwa jinsi gani mwenzako anakupenda. Na ukiona anatetema mdomo basi jua ya kuwa ako na mapenzi zaidi na wewe. Wakati mwingine huchezea nywele yake.

5. Kukugusa wakati anapokuongelesha

Mwanamke anayekugusa huashiria kuwa Ana mapenzi na wewe na hakuogopi. Venye hukugusa huonyesha ishara ya mapenzi na Mara zingine huamua kukumbatia Mara kwa Mara. Wakati anapokumbatia anaonyesha kuwa na wasiwasi kidogo lakini akiona uko sawa anaendelea.

6. Anakufanya ujihisi mwenye furaha.

Mwanamke anayekupenda atahakikisha kila mda unatabasamu. Wanawake hawapendi mwanamme akiwa amekasirika. Akiona umekasirika atajaribu kila namna mpaka aone ukitabasamu.

7. Anapenda kukufuatilia kwenye mitandao

Unapoandika chochote kwenye mitandao Kama vile Facebook, utakuta yeye ni wa kwanza ku comment. Ata like chochote kile uta post kwenye mitandao ya kijamii. Hii pia ni ishara ya mapenzi kwako. Wakati mwingine huamua hata kupost picha yako kwake ili pia aone utakachosema.

8. Anatabasamu kila Mara

Anapokutana na wewe, kitu Cha kwanza hufanya ni kutabasamu hata kabla ya kukuamkua. Hii hutokea hata Kama uko katikati ya marafiki wako. Ina maana haogopi kuonyeshana kwamba ana mapenzi na wewe.

9. Ako tayari kusikia kutoka kwako.

Wataki unapo muongelesha, yeye huonekana akiwa makini sana ili aweze kukuelewa vizuri. Hupenda sana ukimuongelesha. Ukimwambia Kuna kitu ungependa kumwambia Baadaye, Basi yeye atabaki akingoja hayo maongezi. Hii ni ishara moja mhimu sana na mwanamme afaa aelewe kuwa Kuna mapenzi baina yake na huyo mwanamke.

10. Wewe ni mhimu kuliko wengine.

Mwanamke akikupenda, anaweza hata akajificha kwao nyumbani bila hata kujali wazazi wake. Kama amepanga shughuli alafu umwambie wataka kumuona, Basi huenda akaiacha hiyo shughuli ili aje akuone. Akiwa na chochote kidogo, atapenda kugawanya na wewe hata Kama ni chakula. Wakati anapoamka, Basi utakuwa wa kwanza kwenye akili yake. Hapo atafuta namna ya kukujulia Hali hata Kama atapiga simu.

11. Mda wake mwingi ako na wewe

Siku hizi sio watu wengi wako na mda wa kukaa na wengine. Hii ni kwa sababu maisha ni magumu na kila mtu ana shughuli zake za kutafuta hela. Mwanamke anayekupenda hatatatizwa na hayo yote kwani yeye mda mwingi anataka kuwa karibu yako. Hii ni njia moja ya kuonyesha mapenzi kwako. Ukiona mwanamke Kama huyu Basi elewa ana kupenda sana.

12. Anapanga mikutano ya Siri na wewe

Je mpenzi wako huwa anaogopa kukutana nawewe hadharani? Wanawake wengi huchagua kukutana na wewe kisiri ili awe huru kukuongelesha chochote kilicho moyoni. Hii ni ishara ya mapenzi na hangependa yale maneno anayokwambia kusikizwa na mtu mwingine Ila wewe tu.

13. Anapenda kuongea vitu vipya ama mawazo mapya.

Mkikutana naye anapenda kuongea vitu vipya. Anapenda kutoa mawazo tofauti na pia kutaka kujua maoni yako. Akitaka kufanya Jambo lazima akuulizie maoni yako na hutaka ukubali na usipokubali Basi hafanyi.

14. Hapendi ukiondoka

Anapojua wataka kuondoka, atajaribu njia zote ili azidi kukuzuilia maana hataki umuache. Yeye atajaribu kizidisha maongezi na wakati mwingine huanza topic mpya ili azidi kukaa na wewe. Hii ni ishara ya mapenzi na anajua ukienda tu atajihisi mpweke.

15. Mkiongea kwa simu haogopi Ila mkiwa naye anaona haya

Wanawake wengi sana hupenda kuongea na simu kuhusu mapenzi kuliko ana kwa ana. Sio ati anamuogopa Ila Ni tabia za wanawake wengi. Zile vitu huogopa kukwambia mkiwa pamoja huona ni heri atumie simu ya rununu kukueleza.

16. Hukuletea zawadi

Hata Kama ni kidogo, mwanamke hupenda kukupea zawadi kila mnapokutana. Hii ni ishara ya mapenzi na inaonyesha huyu mtu anakufikiria kila Mara. Hukuletea zawadi bila hata wewe kujua yaani ghafla washitukizia ashafika na zawadi.

17. Ana tabia za kitoto.

Hii haimanishi kuwa akili yake haijakomaa. Mara nyingi yeye huhisi vizuri akiongea ama akiulizia vitu vya kitoto. Atakuuliza maswali ya kawaida Kama vile majina ya sehemu, jina ya boss wako na pia ataongea vitu vya kuchekesha.

18. Anapenda kujua maisha yako ya ndani.

Hupenda kujua maisha yako na ya familia yako. Mwanamke anayekupenda huwa ana wivu. Hii inamaanisha atakuulizia hata kwenye ulikuwa Jana usiku. Na pia usipopokea simu pia atataka ajue kwa Nini hukupokea kwa haraka. Maswali Kama hayo huonyesha ishara ya mapenzi Ila sio eti hakuamini.

19. Anataka kukuelewa zaidi

Mwanamke anayekupenda atatafuta namna ya kujua zile vitu wewe wapenda na zile vitu hupendi. Hii Ina maana hataki akufanyie vitu zenye hautapenda na pia anataka akuelewe zaidi. Kama nikivyotangulia kusema mwanamke anayekupenda hapendi kukuona umekasirika na hii ndio sababu ya yeye kujua wapenda Nini na haupendi Nini.

20. Anakumbuka kila kitu chako

Mwanamke anayekupenda atakumbuka kila kitu kuhusu wewe. Chenye ushawahi mwambia, chenye wapenda kula na hata nguo unayoipenda. Kama mwanamke atakumbuka hayo yote Basi mapenzi Kati yenu wawili ni ya kweli.

21. Atakuwa mwaminifu kwako

Kila akitaka kufanya Jambo ama kwenda sehemu atakujulisha. Atahakikisha kwamba unajua alipo na hata anachokifanya. Ukipatikana na shida yote, atakuwa na wewe hadi mambo yako yanyooke.

22. Atakuwa Mvumilivu kwako

Katika mahusiano Mara nyingi hutokea kutoelewana. Wakati mwingine unapokosea mwanamke anayekupenda atakuvumilia na atatafuta namna ili muweze kuelewana.

23. Atakutetea kivyovyote vile

Mwanamke Kama anakupenda Basi atakuwa kwenye mstari wa mbele kukutetea. Huwa hataki kujua Kama una Kosa ama huna Ila hukutetea kwa lolote lile. Mwanamke Kama huyu anaonyesha mapenzi kwako na ako tayari kufa na wewe.

Tazama video mpya ya Zuchu

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *