Maisha

Jinsi ya kumteka mwanamke hisia zake

Wanawake ni viumbe tofauti na unatakiwa uweze kuelewa Jinsi ya kumteka mwanamke hisia zake iii awe mpenzi wako. Wanawake wengi wanapenda nini kwa mwanaume?, Ushawi jiuliza hili swali?

Wanawake wanapenda mwanaume wa aina gani?

Unavyodhani ndivyo, sivyo na huenda ukashangaa sana nikikuambia huu ukweli kuhusu wanawake. Huenda ukafikiria wanawake wengi hupenda wanaume wenye pesa na magari lakini sivyo hata kidogo. Kuna tofauti ya kuwa na hisia za mapenzi na kumpenda mtu ili aweze kuyasukuma maisha yako. Asilimia kubwa ya wanawake walio kwenye uhusiano na wanaume wenye pesa husemekana kutoka nje ya ndoa.

Wengi wa Hawa wanawake hutafuta vijana wadogo na hata watu wa mijengo huku wakidai wanaume wao hawana mapenzi na kila siku wako kazini wakitafuta pesa. Hii ni Jambo hatari sana kwa wanandoa na inamaanisha huyo mwanamke hakuwa na hisia zote za kimapenzi mlipooana ila alikufuata sababu ya pesa zako.

Wanawake wengine hudai hapo mwanzoni mapenzi yalikuwa motomoto ila mambo yakabadilika na mda wa mapenzi ukachukuliwa na shughuli zingine ndio maana wanaona ni heri watafute usaidizi huko nje.

Inasemekana kuwa mapenzi hupatikana kwa familia maskini. Mda mwingi wao huwa wako pamoja na wao huongelea ndoa na familia zaidi ya matajiri. Hii haimanishi basi usiwe tajiri ama usitafute pesa, ni onyo tu ndio uweze kujua kuna changamoto nyingi na unafaa kuwa makini na familia yako na ikiwezekana uweze kutenga mda na familia yako.

Jinsi ya kumteka mwanamke kisaikolojia

Mwanamke anapenda mwanaume anayempa mda. Mwanamke anapenda kusikizwa kila Mara. Hii Ina maana hata akiongea vitu vyenye havina maana, haufai kumlenga unafaa umzikize. Wakati anapotaka kufanya kitu huwa anahitaji maoni yako na usipompa mwelekeo atakasirika. Kama Jambo halifai unafaa kumueleza kwa utaratibu sana usije ukavuruga hisia zake. Tenga mda na mpenzi wako na ikiwezekana mpeleke sehemu tofauti tofauti ili ajihisi tofauti kwani mambo kama haya huyaona makubwa kwake.

Mletee zawadi mwanamke wako hata kama hajaitisha. Mwanamke hachagui kama zawadi yenyewe ni ndogo ama kubwa. Ukiyafanya hayo yote basi utakuwa ushafahamu Jinsi ya kumteka mwanamke kisaikolojia

Dalili za mwanamke anayekupenda ila anashindwa kukwambia

Jinsi ya kumteka mwanamke hisia zake

Wanawake huwa Wana haya za maumbile. Ni vigumu sana mwanamke aje tu akwambie anakutaka. Sio kama wanaume ambao hawana haya na hawaogopi hata kufanya mapenzi hadharani. Kunazo Dalili za mwanamke anayekupenda ila anashindwa kukwambia. Kuzijua mpaka uwe makini sana na uwe unamjua zaidi yule mwanamke. Hizi hapa chini ni baadhi za Dalili za mwanamke anayekupenda.

 • Atakupigia simu kukujulia Hali yako kila mda.
 • Atapenda sana kutembea na wewe.
 • Hukuangalia kwa macho wakati munaongea
 • Anaweza akajinyima kitu Cha dhamani ili wewe upate.
 • Hukuletea zawadi bila hata wewe kuitisha.
 • Atakumbulisha kwa marafiki wake wa karibu na wakati mwingine hata wazazi wake.
 • Atakuchatisha mpaka usiku mnene na hatapenda ukimwambia wataka kutoka online.
 • Asubuhi atakuwa mtu wa kwanza kukujulia hali.

Utajua aje mwanamke hakupendi ama dalili za mwanamke asiyekupenda

Ni rahisi sana, mwanzo atakuwa anakuepuka kila mara. Itakuwa ukijaribu kupiga simu hapokei na hata huenda akaikata haswa. Dalili zingine za mwanamke asiyekupenda ni Kama;

 • Kuku blue tick wanavyosema wasomi. Yaani meseji zako zaingia kwa simu yake ila hajibu.
 • Kila ukimwambia mkutane atatoa sababu zisizo na msingi huenda hata akasema hayupo na unamuona kabisa.
 • Hatawahi kukupigia simu ili akujulie Hali itakuwa wewe peke yako ndiye wapiga.
 • Akikuona tu anasepa hata kama ushamuona.

Jinsi ya kumwambia msichana unampenda.

Usiwahi fanya makosa ya kumwambia msichana unampenda siku ya kwanza kukutana naye. Hata kama kwako utakuwa wamanisha maneno yako, yeye ataona Wamchezea na wataka kumtumia. Jinsi ya kumwambia msichana unampenda hutegemea na kiwango cha urafiki wenu. Mwanamke anapokuwa rafiki basi kumsoma ni rahisi na utaweza kufahamu ni wakati gani unaweza ukamueleza hisia zako. Cha mhimu zaidi ni kwamba usikimbilie na uchukue mda wako kumsoma huyo msichana.

Ninataraji leo umejifunza mengi zaidi kuhusu wanawake na sanasana Jinsi ya kumteka mwanamke hisia zake. Mfanye mwanamke rafiki yako na hayo mengine yataenda yenyewe. Fahamu chenye anapenda na chenye hapendi. Hii itazuia maudhi maana ukija kumuudhi atakuja kukuponyoka. Zidi kufuatilia habari zetu kutoka tovuti yetu ya mwangazanews kwa mafundisho ya Kila siku. Ukiwa na swali unaweza comment hapa chini ili tuweze kuwasilana na wewe. Asenteni kwa kuchagua mwangaza news.

Soma hii pia ( ishara 23 zinazoonyesha mwanamke anakupenda)

 

 

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *