Mchipuko

Kampuni ya Coca-Cola yaongelea kuhusu Coca-Cola girl

Baada ya joy jebiwot kugonga vyombo vya habari. Wakenya wengi waliomba kampuni ya Coca-Cola waweze kumpatia msichana Yule dili ya matangazo.

Leo, kampuni ya Coca-Cola wameweza kuwajibu wakenya na kuelezea Sheria zinazotumika ili tangazo kufanyika.

Kampuni ya Coca-Cola wametoa shukurani kwa mtoto huyo na wakenya kwa jumla kwani jebiwot aliweza kuleta furaha kwa nyuso za watu na kampuni ya Coca-Cola kwa jumla.

” Ni furaha kubwa sana kuona picha nzuri Kama hizi ambapo wakati huu mgumu picha hizi zimeweza kuleta tabasamu kwa wengi.

Ila kampuni hiyo walisema hawawezi kufanya tangazo na mtoto Yule maana hajahitimu miaka kumi na mbili Kulingana na Sheria za matangazo ya kampuni hiyo ambazo zinatumika ulimwengu mzima.

Kampuni ya Coca-Cola

Kampuni yetu ilitoa marufuku ya kuwatumia watoto kwa matangazo na sio hapa tu Kenya mbali inatumika nchi zote ulimwenguni.

” Tumependa ubunifu wa hizo picha na tunaomba mzidi ku share na sisi picha Kama hizo.”

Soma hii pia ( Director wa Tamthilia ya pete ~ Maisha Magic)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *