Mchipuko

Kenya yarekodi visa 123 vya corona kwa mda wa masaa ishirini na nne

Ni mara ya kwanza kwa wizara ya afya kuwahi kutangaza idadi kubwa kama hii Kwa mda wa masaa ishirini na nne. Wizara ya afya imetanga visa 123 vya corona. Hii imetokana baada ya kupima watu 3,007. Idadi hii pia ni kubwa zaidi kuwahi kupimwa kwa mda wa masaa ishirini na nne.

Tangu kutangazwa kwa ugonjwa wa coronavirus nchini kenya, visa vya corona vimefikia 1,471. Kati ya visa 123 vya corona vilivyotangazwa leo, watu 85 wanatokea jijini nairobi huku mombasa wakirekodi visa ishirini na nne. Kiambu wakarekodi visa vinne. County zingine ni pamoja na kajiado visa vitatu, kisumu visa viwili, Garissa,kitui,kilifi, busia na Uasin gishu kisa kimoja kila county.

Health CS Mutahi Kagwe Amref announcement visa 123 vya corona

Kwa sasa Mathare na kibra wanaonyesha kuwa na visa zaidi, Mathare ikifikisha visa 33 na Kibra visa 14. Embakasi North wako na visa 12, Embakasi Central visa vinne, Ruaraka, Kamukuji na makadara visa vitatu kila sehemu, Starehe, Dagoretti North visa viwili kila sehemu. Roysambu, Langata, Embakasi South na Embakasi south kisa kimoja kila sehemu

Soma hii pia ( Willy paul na bahati waanzisha vita upya)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *