Maisha

Karen Nyamu aomba mke wa Samido msamaha

Ni habari ambayo imegonga vyombo vya habari. Karen Nyamu na Samido wamekuwa wakiongelelewa kwa mda mrefu ila juzi ndio mambo yao yaliwekwa hadharani.

Je, karen Nyamu ni nani?

Samido Karen Nyamu

Karen Nyamu ni mwanasiasa na kama umekuwa ukifuatilia siasa basi utakuwa unamfahamu mwanamke huyu. Aliwahi kuwania kiti Cha mwakilishi wa wanawake ( women Rep.) jijini Nairobi. Japo hakuweza kushinda kwenye uchaguzi, bado anaamini kuwa ana uwezo mkubwa kisiasa na ifikapo mwaka wa 2022, atawania kiti Cha kisiasa hata kama ni ubunge.

Samido ni nani?

Samido ni mwanamziki kutoka mkoa wa Kati. Ni msanii anayejulikana ukikuyuni sana kwani nyimbo zake hupendwa sana na wapenzi wa nyimbo za ” Mugithi”. Samido ameoa na ni baba wa watoto wawili. Bali na mziki, Samido ni mwanabiashara.

Uhusiano wa Karen Nyamu na Samido

Uhusiano wao ulianza mwaka wa 2019. Wawili Hawa walikutana kwenye tamasha na wakawa marafiki. Kulingana na karen Nyamu, Samido hakuwahi kumtajia kuwa ameoa. Karen alijua baadae sana kupitia kwa Mc mmoja kwa jina mafirifiri.

Urafiki wa wawili hawa ulipanda cheo na wawili hawa wakaingia kwenye ulimwengu wa mapenzi. Kwa bahati mbaya ama nzuri, karen Nyamu alipata uja uzito wa Samido na baadae kuzaa Mtoto wa kiume.

Karen Nyamu kupitia show ya Jalang’o alidai kwamba amekuwa akimuomba Samido kumtangaza mtoto wake ili watu wajue ako na mtoto lakini Samido amekuwa akihepa hilo Jambo. Baada ya kutoelewana kwa wawili hawa, Karen Nyamu aliamua kuweka wazi tukio lile baada ya ku post video ya Samido na mtoto wao kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hii video ndio iliyoleta mgogangano wa wawili hawa na wanainchi kwa jumla. Wakenya wengi walimkashifu karen Nyamu kwa kitendo alichofanyia huku wakimpa majina ya kila aina. Kulingana na wakenya wengi, karen Nyamu nia yake ilikuwa ni kuharibu familia ya Samido.

Samido kwa upande wake alijitokeza waziwazi na kuamua kumuomba msamaha mke wake kupitia ukurasa wake wa Instagram. Wengi walimsifia Samido kwa hiyo hatua huku wakimpa sifa chemchem kama mwanaume kamili. Samido alikiri kuwa ni kweli ako na mtoto nje ya ndoa ila hajapanga kumuacha mke wake kwa mwanamke mwingine.

Samido's wife

Hii haikuishia hapo. Karen Nyamu alisikika ndani ya Jalang’o Tv akidai kwamba Samido anadanganya. Karen Nyamu alisema Samido alimwambia kwamba mke wake yuajua kuhusiana na huyu mtoto na anaelewa wawili hawa wako kwenye uhusiano. Karen Nyamu aliongeza kusema kuwa anamjua vizuri mke wa Samido na hata ashawahi kumsaidia kwa tender ya pesa nyingi sana.

Karen Nyamu alimuomba msamaha mke wa Samido huku akisema kwamba hakujua kwamba Samido ameoa wakati wakianza uhusiano. Karen alisema hana nia ya kumharibia mwanamke yeyote familia yake kwani yeye pia ni mwanamke na yualewea uchungu wa wanafamilia kuachana.

Soma hii ( kamene Goro anatafuta mwanaume wa kumuoa)

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *