Maana ya tehanani na mengi kuhusu tamthilia hii
Ni wengi sana wamekuwa wakiifuatilia tamthilia hii ila sio wengi wanaojua Maana ya tehanani. Tuliweza kuwasiliana na mwandishi mkuu anyejulikana kama Fakii Kasoloi na kusema kweli ametufundisha mengi tuliyokuwa hatuyajui.
Hii ni tamthilia inayopeperushwa katika kituo cha Runinga Cha Maisha Magic East na Maisha Magic Plus.
Kipindi hiki kilichotayarishwa na Kampuni ya Rhambu Media kinahusu Hadithi ya Ndugu wawili Safari na Fataki ambao wanakuwa maadui baada ya baba Hauna yao kumrithisha Safari mali na kumwacha Fataki ambaye ni mwana wa kambo.
Vita hivi vinamwangukia Haluwa mke wa Safari na Lulu mwanaye wakati Safari anapofungwa jela. Fataki atafanya lolote kupata urithi wake kutoka kwa Haluwa. Inabidi Haluwa ajikaze kiume kulinda jamii yake na Mali ya mumewe dhidi ya Fataki
Maana ya tehanani
TEHANANI maana yake ni TENSION..Hali ya kuwa katika mazingira ya chuki, uhusama na hasira baina watu. Tamthilia hii ni tungo la Fakii Kasoloi Maati na kuandikwa na Fakii Kasoloi na Fatma Kassim.
Tehanani theme song ( Download here)
Mwandishi Fakii Kasoloi.

Mwandishi aliyebobea katika tasnia ya uigizaji na uandishi. Ana miaka zaidi ya 30 ya uigizaji na uandishi hapa Pwani. Katika tamthilia tajika alizoandika ni Kama ALMASI, SUMU, UTANDU, KASHFA, PETE na KAIDI..Katika uigizaji wa hivi karibuni aliigiza Kama Mzee Rajab katika kipindi Cha Nyanya Rukia








Soma hii pia ( Waigizaji wa Maria, Majina na miaka yao kamili)