Mchipuko

Maelezo mafupi kuhusu Turtle (KASA)

Turtle (KASA) Ni mnyama ambaye haliwi Wala kuvuliwa.

Kuna suali liliulizwa kwanini Turtle (KASA) amepigwa marufuku,haruhusiwi kuliwa au kuvuliwa baharini.

minister of tourism watching Turtle (KASA)

Jawabu-
Turtle (KASA) ni aina ya kiumbe kinachoishi baharini,kilichofanya apigwe marufuku ulimwengu mzima na sio kenya pekee,ni kulingana ya mpangilio wa maisha anavyo ishi,kasa huzaa akiwa na umri wa miaka 25,hapo ndio huanza kutaga mayai yake,na mayai yake hutaga nje ya bahari,hutembe ufuoni akajichimbia kwenye mchanga akataga hapo,huchukua mda wa masaa 4 mpaka amalizapo kutaga,na hutoa mayai si chini ya 250.

Amalizapo kutaga hufukia kwa mchanga kiasi na kuregea zake baharini na haregei tena kwenye yale mayai,mayai huchukua siku 60 ndio yakapasuka na watoto kutoka wenyewe,hutoka wakiwa hawajui waendapo,ni wachache mno wanao elekea baharini na wengi hubakia nchi kavu,hapo ndio hukutana na wanyama mbalimbali na aina flani ya ndege kisha wakaliwa wakawa ndio chakula,na wale wanao ingia baharini ambao ni wachache pia huliwa na baadhi ya samaki wakubwa,hivyo kufanya wabakie wakiwa wachache mno,kasa huzaa kila baada ya mwaka mmoja.

Turtle (KASA)

Jinsi ya kujamiana-
Turtle (KASA) hupandwa na dume kwa mda wa siku 7au 8 ,ndie kiumbe wakipekee anaechukua mda mrefu wa kujamiana.

Huu ujumbe umfikie alie uliza swali hili kuhusu kasa, pls share mpaka imfikie.

Soma hii (jinsi ya kupika biriyani)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *