MaishaSanaa

Utajiri wa Rayvanny

Sio wengi hujua kiwango Cha Utajiri wa Rayvanny ilikilinganishwa na wasanii Kama vile diamond platnumz na harmonize. Kuna maelezo mengi kwa mitandao kuhusiana na utajiri wa harmonize na pia utajiri wa Diamond Platnumz Ila tukija kwa utajiri wa Rayvanny huwa kidogo Kuna changamoto.

Rayvanny ambaye jina lake kamili ni Raymond Shaban Mwakyusa pia ni msanii tajiri na apo kwa orodha ya wasanii matajiri nchini Tanzania. Ni msanii aliyepitia maisha magumu kabla hajakutana na Diamond Platnumz. Kusema kweli, Diamond Platnumz amechangia pakubwa sana.

Rayvanny na diamond platnumz
Rayvanny na diamond platnumz

Rayvanny Ni msanii mcheshi na hupendwa sana na watu wengi kwani ukiwa karibu naye itabidi ujitayarishe kucheka.

Rayvanny alianza kujulikana mwaka wa 2016 alipoachia nyimbo yake ya “kwetu” chini ya wasafi. Nyimbo hiyo ilipokelewa vizuri sana na ilimfungulia njia. Nyimbo ya “kwetu’ ilipenya afrika nzima kwa jumla.

Utajiri wa Rayvanny kwa Sasa ni Kati $100,000 na $ milioni moja. Rayvanny hujipatia pesa kutokana na kazi yake ya mziki. Bila mziki Basi hangekuwa tajiri Kama alivyo. Sifa zimuendee Mwenyezi mungu kwa kumkutanisha Rayvanny na diamond platnumz.

Nyimbo zingine za Rayvanny zilizofanya vizuri ni pamoja na Chuchuma, Tetema, Zilipendwa, Zezeta na zinginezo

Rayvanny anamiliki magari ya kifahari na nyumba inayosemekana kugharimu pesa nyingi sana. Pia anazo biashara zinazomuingizia hela zaidi.

Rayvanny wife mke wa Rayvanny
Rayvanny na familia yake

Kwa Sasa bado ako WCB na hivi majuzi alisema hayupo tayari kutoka kwenye label ya wasafi. Ana uwezo wa kufoka,kuimba na kuandika mziki wa kila aina. Kuna wakati aliweza kuwa mshindi wa mtindo huru na hapo ndipo aligundua ako na kipaji.

Kabla hajajiunga na wasafi, Rayvanny alikuwa kwenye label ya Tip Top connection. Hapa ndipo alijifunza mengi inayohusiana na mziki. Akiwa tip top alikutana na wasanii wengi tajika wengi wakimpa mawaidha kuhusiana na swala nzima la mziki

Ni hayo tu kwa leo kuhusiana na utajiri wa Rayvanny. Zidi kufuatilia taarifa za mwangaza news. Usisahau ku subscribe kwa mengi zaidi kwa kubofya kengele nyekundu ilioko pale chini pembeni upande wa kulia.

Soma hii pia (watu matajiri duniani)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *