MchipukoSanaa

Marina Joyce ni nani na nini kilimfanyikia?

  • Marina Joyce aliwahi kuripotiwa kutoweka baada ya kuonekana mara ya mwisho 31 july 2019 nyumbani kwake london lakini Baada ya siku tisa alipatikana.

Marina Joyce ni nani?

Ana miaka ishirini na mbili, alizaliwa sehemu inayojulikana kama Haringey ilioko London Alianzisha youtube yake mwaka wa 2010 na kwa sasa ina subscriber zaidi ya millioni mbili.

Marina Joyce hutengeneza video za youtube zenye mafundisho ya jinsi ya kufanya vitu tofauti tofauti. Pia hufanya video za urembo na hufundisha watu jinsi ya kujirembua.

Kwenye mitandao, Marina Joyce hujiita sacred moon snowflake cat princess of love. Video yake ya mwisho kuieka kwa youtube channel yake ilikuwa kuhusiana na jinsi ya kusafisha nywele na kuichunga kutokana na makali ya chemikali. Video hiyo aliipatia jina la, “How i care my hair”

Katika ile video yake aliweza kusema kuwa ataachia video nyengine alhamisi iliyofuatia lakini haikufanyika kwani alitoweka. Post yake ya mwisho kwenye facebook ilikuwa tarehe 24 kuhusu biashara zake.

Fashion Vlogger Marina Joyce

Marina Joyce alipotea lini?

Alitangazwa kupotea mnano tarehe 31 july 2019. Mara ya mwisho kuonekana alikuwa anatoka kwake nyumbani ila haijulikani alimokuwa akienda. Kikundi cha the missing people charity kilieza kuweka matangazo kuhusiana na mwana youtube Marina Joyce.

Waliweza kutoa ujumbe na kuandika, na pia wakaeka number ya simu ili yeyote aliye na habari kumhusu mwanadada huyu aweze kuwatumia ujumbe mfupi ama aweze kuwapigia simu ili waweze kumfuatilia alioko Marina Joyce

“…..Marina tuko hapa na tupo tayari kukusikiza….. chochote kile unataka tutakusaidia, tafadhali jitokeze…yeyote atapata habari kumhusu aweze kutujulisha…..”

Polisi wa metropolitan waliweza kuanzisha msako wa mwanadada huyo kwani mnamo august saba, Marina Joyce alilipotiwa kwenye Kituo cha polisi cha Halingey

Marina Joyce alipatikana lini?

Kituo cha polisi cha Halingey kiliweza kutoa ripoti kuwa wamempata akiwa buheri wa afya.. ujumbe huu waliweza ku post kwa twitter na kusema

” Tuliweza kuomba usaidizi kufuatia kutoweka kwa Marina Joyce ila kwa sasa tumempata na tunashukuru bidii ya kila aliyehusika….

Soma hii pia ( Huenda tanasha akaanza mahusiano mapya)

 

 

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *