Maisha

Teacher Wanjiku aamua kufuata nyayo za Babu Owino

Teacher Wanjiku aamua kufuata nyayo za Babu Owino na kuazisha masomo ya mtandao. Kama umekuwa ukifuatilia, Babu Owino alianzisha masomo ya mtandao na kwa sasa ako na wafuasi wengi wanaojifunza kupitia kwa ujuzi wake.

Teacher Wanjiku ni mzazi na ana watoto wawili. Tofauti na Babu Owino, yeye ameamua kufunza watoto wa chekechea na sana sana anazingatia Letter sounds. Kulingana na yeye, anataka wazazi pia waelewe haya masomo kwani kuna tofauti kubwa kwa masomo ya sasa na ya hapo awali.

Leo aliweza kueka video kwenye mtandao wake wa Instagram huku akionyesha tofauti ya vile mafunzo yapo kwa sasa na yalivyokuwa hapo awali wakati yeye alikuwa shuleni. Alijaribu kuonyesha vile mwalimu wake alimfunza na vile walimu wa siku hizi wanavyofunza.

Teacher Wanjiru wedding
Teacher Wanjiru ni mumewe wake kwenye harusi yao

” Kama wewe ni mzazi, nakuhisi uweze kujifunza namna yakutamka A-Z, mimi ninaye mtoto wa miaka minne na huu mda tumekuwa tukipitia pamoja na naweza kusema nimejifunza mengi….”Alisema Wanjiku

Teacher Wanjiku alisema amehakikisha chenye anafundisha kwa mitandao kimeidhinishwa na CBC na anafuata maagizo yao kwa hivyo anafunza inavyotakikana. Wengi walimsifia sana na wakagundua kumbe walichofundishwa ni tofauti na masomo ya sasa.

Tofauti nyengine yake na Babu Owino ni kwamba, Babu Owino anafundisha Chemistry na Biology ila yeye ameamua kufunza watoto wa chekechea. Yaonekana wazazi wengi waliweza kufuatilia mafundisho kwani kulingana na video aliyo weka kwa instagram, wengi waliweza kuitazama.

Kulingana na wengi, Masomo ya hapo awali yalikuwa rahisi ikilinganishwa na ya sasa. Hawajajua ni kwa nini kulitokea mabadiliko kwa masomo ya sasa.

Soma hii pia ( Sikuamini alichokifanya Size 8 : Bien sauti sol asema)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *