Maisha

Mbinu za kufaulu maishani

Je, ungependa kuzijua Mbinu za kufaulu maishani. Wakati mwingine maisha huenda ikakwendea vibaya na hata ukakosa hamu ya kuishi. Matokeo kama haya huletwa na mambo mengi ikiwemo kutofanikiwa maishani.

Asilimia kubwa ya wanaojutia maisha yao ni wale ambao labda hawakujipanga hapo awali na ndio maana maisha yao ikawa ya majuto tele. Kuna wengine walijipanga ila mambo hayakuenda kama walivyotegemea. Unaweza ukajipipanga kimaisha ila vitu vikatokea ghafla na maisha yako ikakugeuka na kuwaacha watu vinywa wazi kwa kuona mambo yako yakabadilika ghafla.

Mbinu za kufaulu maishani

  • Kupanga uzazi
  • Kuekeza
  • Kujipanga kimaisha
  • Kumrudia mungu
  • Kuanzisha miradi

Kupanga uzazi

Kupanga uzazi | Family planning

Ni Jambo linaloonekana kuwa la kawaida Ila usipolijulia huenda maisha yako yakaharibika. Kupanga uzazi kunachangia sana kufaulu maishani. Kuwa mzazi sio kazi rahisi maana malezi ya watoto yategemea sana mapato yako.

Kama kipato chako kipo chini basi na una familia kubwa, basi huenda ukaumia. Kumbuka familia yako yakutegemea wewe hii Ina maana wakati unafikiria kuongeza kizazi, lazima ufikirie kwanza kama utaweza kuwalisha na pia kuwapewa mahitaji ya kila siku.

Ikiwa utashindwa kuwalea watoto wako Basi maisha yako yatatatizika na kama ni kufaulu itakuwa ni ndoto. Kumbuka kupanga uzazi ili uweze kufaulu maishani.

Kuekeza

Raha za dunia huenda zikakutatiza na ukasahau kwamba kuna maisha ya baadae. Watu wengi sio kwamba hawana uwezo wa kujikimu kimaisha ila mda wanapokuwa wanapokea hela wakati wako kazini ama biashara zao, wanasahau kuekeza. Kila kitu kina mwanzo na mwisho, leo waweza kuwa una kazi nzuri na unapokea pesa nzuri ila kesho kazi ikaisha na ukabaki kuombaomba kama hukujipanga. Jaribu sana kuwekeza ili baadae usije ukajuta.

Kujipanga kimaisha

Je pesa zako unazitumia kivipi, kuna watu wanapata pesa kidogo ila wamejiekea matumizi mengi kuliko kipato chao. Kama kipato chako ni kidogo jaribu kupunguza matumizi. Kwa mfano unalipwa pesa kidogo alafu badala ya kupika chakula nyumbani, wewe na familia yako mnaamua kula hotelini. Utafiti wetu unaonyesha watu wenye wanatumia pesa bila mipangilio huishi maisha mabaya hapo mbeleni

Mfano mwingine ni wakati unaishi pekee yako lakini unaishi kwa nyumba ya bedroom mbili tena ya kukodisha. Hapo utakuwa unapoteza pesa. Jaribu kujipanga kimaisha na uache kutumia pesa bila mipangilio.

Kumrudia mungu

Katika maisha haya ya leo usiwahi msahau mungu kwa chochote kile unachokifanya. Kumbuka mungu ndiye anawezesha kila Jambo na bila yeye mambo yako hayawezi kunyooka. Omba mungu wakati wowote ule. Sio lazima uwe unampa mungu mahitaji yako ndio umuombe, wakati mwingine unafaa kushukuru kwa yale Mungu amekufanyia.

Soma hii pia (Jinsi ya kumteka mwanamke kisaikolojia)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *