Mchipuko

Mzee Abdul sio babake diamond platnumz, mama dangote afichua siri

  • Mzee Abdul sio babake diamond platnumz, mama dangote afichua siri

Baada ya miaka mingi ya msanii wa Bongo Flavor Diamond Platnumz kulaumiwa kwa kutomsaidia babake Mzee Abdul, hatimaye Mamake mzazi Bi.Sandra amejitokeza na habari za kushangaza kuwa Mzee Abdul sio babake diamond platnumz.

Mamake Diamond Platnumz maarufu kama Mama Dangote amejitokeza na kudai kwamba Mzee Abdul sio baba halisi wa Diamond na kwamba walipatana wakati tayari alikuwa na ujauzito wa Diamond.

“Alinipata nikiwa tayari na ujauzito wa Diamond, nikamwambia tulee mtoto pengine atakuja kusaidia mbeleni lakini baadae hakutaka kushughulika.. Yeye ni baba mlezi tu lakini sio Babake mzazi” Amesema Mama Dangote.

Kupitia kipindi cha radio cha #Masham_Sham ndani ya Wasafi Radio, Mama Dangote amedai kwamba babake halisi wa Diamond ni jamaa anajulikana kama Salum Iddi Nyange ambaye pia ndie babake Ricardo Momo.

Baada ya ufichuzi huo, Mzee Abdul amehojiwa na wanahabari lakini kwa upande wake amekana madai kwamba alimpata na ujauzito na kusema ujauzito wa Diamond ulipatikana wakiwa tayari wameoana, na habari za leo kwamba sio mtoto wake pia yeye amezipokea kwa mara ya kwanza kama watu wengine.

Hata hivyo Mzee huyo amemshukuru Mama Dangote kwa kuibua ukweli huo na kumuomba Diamond Platnumz aliondoe jina la Abdul katika vyeti vyake, kama anavyoitwa sasa Nasib Abdul.

“Mara nyingi nimekuwa nikimuomba Diamond msaada ananinyima sikujua kumbe wenyewe walikuwa wameongea na Mamake. Mimi sina shida nimeshukuru, mimi sasa sio Babake Diamond” Amesema Mzee Abdul.

Mama Dangote baadae amepost picha ya Mwanaume katika ukurasa wake wa Instagram kwa mara ya kwanza muda mfupi uliopita bila Caption yoyote huku wengi wakiamini huyo ndiye huyo Mzee Salum Idd, babake halisi wa Diamond aliyekuwa amemtaja hapo awali.

Soma hii pia ( wanawake warembo Tanzania)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *