InternationalMaisha

Mishono ya vitenge

Kitenge ni vazi ambalo bado lipolipo hata kama ni vazi la kitambo. Mpaka sasa vazi hili linazidi kupendwa na kutumiwa sana haswa hapa afrika. Vazi la kitenge hutumika sana katika sherehe nyingi hapa afrika.

modern Kitenge design for long dresses

Kunao mafundi wengi wa mshono wa kitenge. Kila kukicha wanazidi kufumbua mishono ya vitenge ya kila aina. Vitenge hushonwa Kulingana na sherehe unayotaka kuhudhuria. Kuna mafundi wanashona nguo nzima yaani full dress kitenge, skirts na hata shati.

Kama unataka kufanya harusi ya kitamanduni ama ya kisasa, basi usijali maana utashonewa kitenge chako Kulingana na sherehe yenyewe na vile utakavyo. Kama unataka kushonewa kitenge unafaa mwanzo utafute muundo ama design. Katika mitandao wa pinterest utapata design nyingi sana za aina za vitenge. Kuna mafundi wengine tayari wamekuwa wakishona vitenge kwa miaka mingi na wanazo design wanaweza kukuonyesha ili uweze kuchagua.

Wakati unavaa nguo yoyote, huwa inasema mengi kuhusu na mtu akikutazama anafaa kusoma mengi kuhusu.

 

nigerian Kitenge designs

Mishono ya vitenge

Mishono hutegemea na chaguo la mtu anayetaka kushonewa. Kuna wanawake wanapenda nguo ndefu na kuna wengine wanapenda nguo fupi. Wanaume wengine nao hupenda mchanganyiko na wengine wanapenda wawekewe kiasi kidogo tu kwa nguo zao. Kwa kweli mishono ya vitenge ni mingi sana na unaweza pata vazi aina yoyote kutokana na vitenge.

mishono ya vitenge vya kisasa

Unapowatembelea wazazi wako unastahili kuvaa kiheshima. Hawa wazazi wanaweza kuwa ni wakwe zako ama wazazi wako rasmi. Kumbuka watakavyokuona wakwe wako kwa siku ya kwanza ndivyo watakuchukulia kwa hivyo hakikisha unavaa vizuri.

 

Kama unafanya harusi, unaweza amua badala ya kuvaa mavazi ya kisasa, uamue tu wewe na timu nzima mvae kitenge. Harusi kama hizo hupendeza sana na huonekana na mpangilio mzuri kwani zinazingatia tamanduni za waafrika. Kuna watu wengi tajika washatumia vazi la kitenge kwa harusi zao na harusi yao ikawa ya kupendeza.

Vitenge vya kisasa

latest Kitenge design for ladies

hata kama tulitangulia kusema kuwa vitenge ni mavazi ya zamani, kunazo vitenge vya kisasa. Kadri maisha yanavyosonga ndio nao mafundi wanazidi kufumbua miundo zaidi. Kuna mafundi wakiamua kushona vitenge na miundo ya kisasa hautaamini kwani Wana uwezo mkubwa sana.

mishono mipya ya vitenge

latest Kitenge design in kenya

Kwa wakati huu unaweza pata aina nyingi za vitenge madukani. Kumbuka kawaida ya biashara yoyote ile kuna ushindani kwa hivyo kila anayehusika na hii biashara ya vitenge anajaribu kufanya kitu bora zaidi kumshinda mwenzake. Unaweza ukaitazama mishono zaidi ya vitenge hapa chini labda huenda ukaipenda.

mishono ya vitenge magauni marefu

mishono ya vitenge magauni mafupi

Vitenge vya nigeria.

Wa nigeria wanasemekana kuwa wakali kwa mishono ya vitenge. Vazi hili linatumika sana nchini humo maana hata waigizaji wanalitumia. Vitenge huvaliwa kwenye aina ya Sherehe nyingi nchini humo. Tazama mishono tofauti ya vitenge nchini Nigeria.

Soma hapa pia ( faida ya majani ya mapera)

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *