InternationalMzikiSanaa

Top 10 ya Wasanii tajiri africa Kulingana na forbes

Top 10 ya Wasanii tajiri africa Kulingana na forbes

Kama Kazi nyingine ile, kwenye Sanaa, mziki unaweza ukakuletea mapato makubwa sanasana kama una ufahamu mkubwa kuhusiana na Sanaa ya mziki. Hii imedhihirika wazi kwani wengi wa wanamziki wamefaulu zaidi duniani kote. Ukitazama orodha ya wasanii tajiri Afrika utaipata picha vizuri

Wakati unapokutana na watu wakiulizia kuhusu wasanii tajiri Afrika, je ni msanii gani huja kwa akili yako? Wengi huchagua wanamziki wanaofanya bora kwenye Sanaa ya mziki kama wanamziki tajiri zaidi.

Sanaa ya mziki ndani ya afrika ipo na ushindani mkubwa sana hivyo msanii mwenye uwezo na kinachohitajika kwenye Sanaa ndiye hupata nafasi mwafaka ya kufaulu kwenye mziki.

Msanii huyo lazima pia awe na talanta kwani bila talanta itakuwa ni vigumu kufaulu. Kwa vile wasanii ni wengi kote duniani, ni lazima uwe na uwezo mkubwa na kitu flani tofauti ili uweze kuwapita wengine na kuwa kwenye nafasi bora.

Kwa kuongezea, wasanii walioketi sana kwa Sanaa ya mziki hupata mapato zaidi kwani tayari washatengeneza jina. Wasanii kama hawa hupata nafasi hata ya kusafiri nchi za nje na kusema kweli, hurudi na pesa ya kisawasawa.

Katika hii orodha ya wasanii tajiri Afrika ni wasanii wenye washawahi fanya mambo makubwa kwenye Sanaa ya mziki. Kusema kweli ni kwamba bidii yao imewafanya kupata mapato makubwa kwenye mziki. Wasanii kama hawa kwa sasa wanaishi maisha ya kitajiri.

Ili uwe kwenye list ya wasanii tajiri Afrika lazima uwe na uwezo wa kusambaza mziki wako kutumia njia inayofaa kama vile mitandao. Kwenye mitandao lazima uwe na wafuasi wengi kwani wakiwa wengi, mziki wako utaweza kuwafikia hivyo basi utazidi kujulikana.

Kuna wasanii wengine huamua kushikana pamoja ili waongeze nguvu kwani kama mjuavyo umoja ni nguvu.

Ifuatayo ni orodha ya wasanii tajiri Africa.

1. Youssou N’ Dour – net worth $145

Youssou N’Dour net worth $145 million

Majina yake ya kuzaliwa anafahamika kama Youssou Madjiguéne Ndour. Alizaliwa nchini senegal tarehe 1 October mwaka wa 1959. Anaimba, anaandika nyimbo, ni muigizaji, mwanabiashara na tena ni mwanasiasa.

Alianza usanii akiwa na miaka 12. Miaka ya 70s’, alitumbuiza pamoja na Band tajika ya huko Dakar kwa jina maarufu ‘The star Band’ . Youssou ana sauti ya kuvutia na aliwahi kutangazwa kama msanii anayejulikana zaidi nchini senegal.

Amewahi shinda tuzo za msanii tajika na msanii tajiri kwa miaka kadhaa na Anajulikana kama msanii tajiri Afrika.
Utajiri wake unasemekana kuwa millioni $145. Youssou anamiliki kituo Cha utangazaji kinachosemekana kuwa kikubwa sana nchini senegal. Kituo hiki kina radio na pia Tv. Pia ako na estate kwani kama nilipotangulia kusema ni mwanabiashara na ana dili na “Real estates”

2. Akon – net worth $80 million

Akon net worth $80 million

Kwa majina kamili Anajulikana kama Aliaume Damala Badara Akon Thiam. Alizaliwa April tarehe 16 mwaka wa 1973. Yeye pia ni mwananchi wa nchi ya senegal japo maisha yake ameishi america.

Ni msanii mwenye talanta ya hali ya juu na amekuwa kwenye mziki kwa miaka mingi sana. Bali na kuwa mwanamziki, Akon pia ni muigizaji na pia mfanyi biashara.

Ni msanii anayesemakana kuwa na ujuzi mkubwa sana wa kuwekeza na ndio chanzo Cha utajiri wake. Kwa sasa ameshikilia nafasi ya pili kama msanii tajiri Afrika. Utajiri wake unasemekana kuwa $80 million.

Kama mmoja wa wasanii tajiri Afrika, Akon anaandika nyimbo na pia anazitayarisha mwenyewe yaani yeye pia ni “music producer”. Kampuni yake ya kutayarisha mziki pia inajihushisha na kutengeneza matangazo ya biashara hivyo kuongeza mapato.

Ako ana label mbili za mziki zikiwemo label ya konvict muzic na Kon Live distribution. Kama umekuwa ukifuatilia Sanaa basi utakubaliana na Mimi kwamba hizi ni label kubwa sana duniani.

Katika label yake, Akon ako na mkataba na wasanii tajika kama vile T-pain na Lady Gaga. Wasanii Hawa wawili wanamuingizia Akon hela ndefu sana kwani majina yao yapo juu ulimwengu mzima.

Bali na afrika, Akon ana wafuasi wengi sana duniani kote. Hadi sasa msanii huyu ameuza zaidi ya album 35 million. Ashawahi chagulia kupigania tuzo za grammy awards Mara kama tano. Nyimbo zake zaidi ya 45 zimepata nafasi Kati ya zile nyimbo Kali ndani ya Billboard Hot 100 songs. Talanta yake inazidi kumpa jina zaidi na hadi sasa anajulikana ulimwengu mzima.

3. Black Coffee – $60 million

Black Coffee dj net worth $60 million

Majina kamili Anajulikana kama Nkosinathi Maphumulo. Ni msanii kutoka nchi ya afrika kusini. Ni msanii wa tatu kwenye orodha ya wasanii matajiri afrika. Alizaliwa mwaka wa 1976, March 11 katika sehemu inayojulikana kama Umlazi nchini Afrika kusini. Utajiri wake ni $60 million.

Anatambulika kama msanii aliyewahi kushinda tuzo nyingi. Sio south africa tu, msanii huyu Anajulikana kote duniani. Ni msanii mbunifu sana na kila anapotumbuiza watu hufurahia sana.

Mwanamziki huyu alianza usanii mwaka wa 1995 baada ya kuachilia album tano kutoka kwa label yake. Alijulikana zaidi mwaka wa 2004 alipochaguliwa kuwa katika Red Music Academy iliyofanyika cape town.

Mwaka wa 2005 alishinda tuzo za DJ awards ndani ya Ibiza kama Dj ambaye amefaulu zaidi. Anamiliki magari ya kifahari kama vile mercedes Benz, G station Wagon, CLK mercedes, Bentley na maserati. Pia anayo private jet.

4. Davido – $40 million

Davido net worth $40 million

Kwa majina kamili Anajulikana kama david adedeji adeleke. Aliziwa atlanta georgia November tarehe 21 mwaka wa 1992. Anajulikana kwa mziki wake mzuri unaopendwa na kuchezwa Kila sehemu. Davido hadi sasa amepata tuzo nyingi sana na pia kampuni nyingi zinamlipa kwa kumtumia kwenye matangazo yao ya biashara.

Kulingana na forbes, label ya davido kwa jina DMW inaleta hela nyingi sana. Msanii huyu ana utajiri wa zaidi ya $40 million. Davido alikuwa akiufanya mziki kama mchezo tu ama kwa kizungu “hobby” lakini kwa vile mziki wake unapendwa akaamua kufanya mziki kama biashara.

Ilimchukua miaka kidogo sana kwa davido kuweza kufika mahali amefika kwa sasa. Mwaka wa 2011 ndio ulikuwa mwaka wake baada ya kuachia nyimbo yake ya “Back” baada ya hapo jina lake lilipanda na akajulikana zaidi ulimwengu mzima.

Alizidi kulipandisha jina lake kwa kufanya colabo na wasanii tajika kote duniani. Alipanga maonyesho mengi Nchi mbalimbali na upendo kutoka kwa mafans wake ulizidi na ikawa ni rahisi kwake kupata pesa nyingi kupitia mziki wake. Hadi sasa, davido bado ako juu kwani anazidi kufanya mziki mzuri na watu wanapenda sana mziki wake.

5. Wizkid – net worth $30 million

Wizkid net worth $30 million

Kwa majina kamili Anajulikana kama Ayodeji Ibrahim Balogun. Ni msanii ambaye ana talanta na anaweza kufanya mziki wa kila aina. Ni raia wa nchi ya nigeria na alizaliwa June tarehe 16 mwaka wa 1990. Ni mmoja wa wasanii tajiri nchini nigeria.

Utajiri wa Wiz Kid ni $30 million. Nyimbo yake ya holder iliwahi kuwa namba moja ndani ya Top Hot 100 Songs, Top R&B song na pamoja na Top R&B collaboration Awards. Mafans wake humuita Mfalme wa mziki wa afrika kwani anapoachia nyimbo huwa ni ‘hit’

6. Don Jazzy – net worth $17.5 million

Don Jazzy net worth $17.5 million

Kwa majina kamili Anajulikana kama Michael collins Ajereh. Alizaliwa November tarehe 26 mwaka wa 1982.

Cha maajabu, Don Jazzy hana nyimbo kama yeye ila utamsikia kwa nyimbo za wasanii wake. Ni msanii mkubwa na mwenye pesa nyingi africa. Ni mtayarishaji wa mziki, anaandika nyimbo na pia ni mwanabiashara.

Utajiri wake kwa sasa ni $17.5 million. Ameshinda tuzo nyingi sana ashawahi kuwa ambassador wa MTV.

Record label yake imewasaidia wanamziki wengi chipukizi na bali na mziki, don Jazzy anajihushisha na biashara ya “Real Estate” pia anajihushisha na usambazaji wa “Wi-Fi nchini nigeria.

7. Rudeboy – net worth $16 million

Rudeboy net worth $16 million

Alizaliwa November 18 mwaka wa 1981, kwa majina kamili ni paul okeye. Huyu ni mmoja wa wasanii 10 tajiri Afrika.

Paul na mwenzake peter ambao ni mapacha waliwahi kuwa kwa group moja ya mziki kwa jina P-square. Wakiwa wawili waliheshimika sana na walitajika kama wasanii waliofaulu nchini Nigeria.

Mwaka wa 2017, wawili hawa, waliachia album ya pamoja. Baada ya miaka kumi na tano pamoja, kila mtu aliamua kwenda kivyake. Na sasa Kila mtu anarekodi mziki kivyake.

Wakiwa wawili walikuwa na utajiri wa $150 million kabla hawajaachana. Baada ya kugawanya mali zao, Rudeboy akabaki na utajiri wa $16 million.

Rudeboy anamiliki nyumba ya kifarahi katika maeneo ya parkview estate lagos nchini Nigeria. Anayo magari ya kila aina.

8. 2Baba aka 2Face Idibia – net worth $15 million

2Baba aka 2Face Idibia net worth $15 million

Majina kamili ya 2 Face ni innocent Uja Idibia. Alizaliwa September kumi na nane mwaka wa 1975 nchini Nigeria.

Ni muigizaji, mwanamziki, mtayarishaji wa mziki na pia anaandika sana mziki. Alianza akiwa mmoja wa kikundi Cha Nigerian R&B group plantashum boyz. Mwaka wa 2006, alipata umaarufu zaidi baada ya kuachia nyimbo ya African queen iliyomuingizia hela zaidi.

Ameuza album zaidi ya saba na ashawahi shinda tuzo zaidi ya 40. Kama wasanii wengi wa nigeria, 2 face pia anajihushisha na biashara ya Real estate. Yeye ni brand ambassador wa pazino homes and gardens.

Mwaka wa 2009 alichaguliwa kama ambassador wa National Agency for food and drug administration and control. Haikuishia hapo kwani mwaka wa 2020 alichaguliwa ambassador wa UNHCR ( The UN Refugee Agency)

Pia aliwahi kupata dili ya guinness iliyomuingizia $125,000 na pia siku ya Airtel iliyompa $139,000. Kwa sasa utajiri wake ni $15 million.

9. Mr. P – net worth $11 million

Mr. P net worth $11 million

Kama niliposema hapo awali, huyu ni pacha wake paul Rudeboy. Kwa majina kamili Anajulikana kama peter okoye. Yeye na kakake wako katika orodha ya wasanii tajiri Afrika.

Mr. P anazo project nyingi ikiwemo tv show tajika kwa jina “Dance with Peter”. Ameachia nyimbo nyingi sana na hizo nyimbo zinamletea pesa zaidi. Mr. p hufanya matangazo ya biashara ( adverts) zinazomuingizia hela zaidi

Ako na nyumba ya kifahari inayosemekana kuwa gharama yake ni 2 billion Naira. Ana magari mengi ya kila aina. Utajiri wake ni Kama $11 million.

10. D’Banj – net worth $11 million

Pia Anajulikana kama Koko master. Ni msanii maaruufu nchini nigeria. Anaandika nyimbo, ni mtangazaji kwenye television na pia ni mfanyi biashara. D’Banj alizaliwa June 9 mwaka wa 1980. Kwa majina kamili Anajulikana kama Dapo Daniel Oyebanjo.

Msanii huyu ameshinda tuzo kadhaa. Alikuwa mwanamziki wa kwanza afrika ku sign mkataba na Kanye West katika label yake ya Good Music Label. Alimfanyia kampeni rais Jonothan Goodluck. Ako na club za kifahari na kubwa sana nchini Nigeria.

Orodha ya Wasanii tajiri Afrika 2021

  1. Youssou N’Dour – net worth $145 million

  2. Akon – net worth $80 million

  3. Black Coffee – net worth $60 million

  4. Davido – net worth $40 million

  5. Wizkid – net worth $30 million

  6. Don Jazzy – net worth $17.5 million

  7. Rudeboy – net worth $16 million

  8. 2Baba aka 2Face Idibia – net worth $15 million

  9. Mr. P – net worth $11 million

  10. D’Banj – net worth $11 million

Afrika kuna wasanii wengi wenye vipaji. Wasanii hawa Wana uwezo wa kufanya mziki wa kila aina. Wasanii tajiri Afrika Wana talanta ya hali ya juu. Sio kirahisi kufaulu kwenye mziki ulio na ushindani mkubwa ila ni kwa bidii. Bidii yao yenye imewapa majina makubwa na kwa sasa ni matajiri barani afrika.

Tazama hapa chini wasanii tajiri Tanzania

Soma hii pia ( wasanii tajiri duniani)

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *