MchipukoSanaa

Orodha ya wasanii matajiri tanzania 2021

Orodha ya wasanii matajiri tanzania 2021 ni tofauti na ya mwaka wa 2021 na kusema kweli orodha hii huenda ikibadilika kila kuchao.wasanii kutoka tanzania wanasemekana kutengeza pesa nyingi kwenye sanaa. Nchi ya tanzania inasemekana kupata kipato kikubwa kupitia Sanaa. Tanzania inajivunia kuwa na wasanii wengi wenye vipaji. Wasanii wa Tanzania Wana bahati sana kwani serikali ya rais magufuli anawapa sapoti sana.

Najua ni wengi wamekuwa wakitamani kujua viwango vya wasanii matajiri tanzania na pesa walizonazo kwenye benki. Ifuatayo ni orodha ya wasanii tajiri tanzania iliyofanyiwa utafiti wa Hali ya juu

Orodha ya wasanii matajiri tanzania

Diamond platnumz – $ 8 million

Diamond platnumz - $ 8 million

Diamond platnumz ni msanii anayetokea tanzania. Bali na mwanamziki, msanii huyu ni mwanabiashara, ni mchezaji ngoma na pia ni meneja wa wasanii karibia watano walioko WCB. Alizaliwa tandale dar es salaam, anamiliki wasafi FM wasafi Tv na pia ni meneja wa WCB. Kwa sasa msanii huyu ana utajiri wa dollars $ 8 na inaonekana mwaka ujao atazidi kuingiza hela zaidi.

Harmonize – $ 6 million

Harmonize - $ 6 million

Kama kuna msanii anatikisha wasafi ni harmonize. Baada ya kujitoa kwenye management ya wasafi, harmonize anafanya vizuri na anazidi kuingiza hela zaidi. Mziki anajua na tunaweza sema labda amejifunza kutokana na aliyekuwa meneja wake diamond platnumz. Harmonize ana majumba ya dhamani kubwa sana na magari ya kifahari. Kwa sasa anamiliki label ya konde gang huku akiwa na wasanii kadhaa Kama vile ibra na county boy. Utajiri wake umetokana na kuuza mziki kwenye mitandao na performance katika maeneo mbalimbali ulimwengu. Mke wa harmonize Sarah amechanga pakubwa katika kufanikiwa kwake. Inasemekana familia ya Sarah mkewe harmonize wanajihushisha na biashara ya kutayarisha na kuuza madini.

Alikiba – $ 5.5 million

Alikiba - $ 5.5 million

Ni msanii mkubwa pia nchini tanzania na baada ya diamond platnumz, alikiba anashikilia nafasi ya pili. Wengi wanapenda mziki wa alikiba kwani wadai japo yeye huchukua mda kabla ya kuachia nyimbo mpya, msanii huyu anafanya mziki wa kuishi kwa mda mrefu. Kama diamond platnumz, alikiba pia ni mchezaji ngoma. Ni mwandishi mzuri sana na pia ni muigizaji katika sinema. Alikiba hupenda kuficha maisha yake na hueka Siri sana mafanikio yake. Kiwango cha utajiri wake ni Kama $ 5.5 anazozipokea kutokana na kuuza mziki wake na copyright. Ukitaka alikiba aweze kutumbuiza kwa sherehe yako basi inakubidi uwe na zaidi ya $ 4,000.

Professor Jay – $ 4.5 million

Professor Jay - $ 4.5 million

Majina kamili Anajulikana kama joseph haule. Ni mmoja wa wasanii wakongwe. Ashawahi kuwa mbunge wa mikumi constituency ila mwaka Jana alipoteza nafasi hiyo na huenda akarudi kabisa kwa mziki. Professor Jay ni mwandishi mkali wa mziki aina ya hip-hop.

Lady jaydee – $ 4.2

Lady jaydee - $ 4.2

Kwa majina kamili judith wambura mbibo. Kama professor Jay, lady jaydee ni msanii mkongwe mwenye sauti ya kutoa nyoka pangoni. Msanii huyu pia ni mwanabiashara na mwandishi mzuri sana wa mashairi. Wasanii wakike wanaoibuka hivi sasa kama Nandy na zuchu wanamheshimu sana maana yeye ni mmoja wa wasanii wa kike walioanzisha Sanaa. Lady jaydee ako kwenye label ya Taurus music na wengi wanamjua kama malkia wa bongo flava ( queen of bongo flava)

Rayvann | Vanny boy – $4.1 million.

Rayvann | Vanny boy - $4.1 million.

Ni katika wasanii wale wa mwanzo waliosajiliwa ndani ya wasafi label punde tu label hiyo ilipoanzishwa. Kufikia sasa msanii huyu anajipatia kipato kikubwa sana na nyimbo zake zimepenya zaidi. Kumpata Rayvann kwa show yako itabidi mfukoni uwe na zaidi ya $ 3,000. Utajiri wa Rayvann unatokana na uuzaji wa mziki kwenye mitandao na pia kwenye show anazozifanya ndani ya tanzania na nje ya nchi yake.

Zuchu – $ 4

Zuchu - $ 4

Ni msanii mpya kwenye label ya wasafi. Kusema kweli msanii huyu amefanikiwa kwa mda mfupi sana na saa hii anakimbizana na wasanii wenzake ndani ya wasafi record. Zuchu ameanza kupiga show na mziki wake unauza sana kwenye mitandao. Ni juzi tu yeye na Rayvann walienda kuchukua pesa zao za download na zuchu alinukuliwa akisema walipata hela ndefu sana. Kwa mda mfupi, Zuchu ameingia kwenye orodha ya wasanii matajiri tanzania. Kwa sasa ana video kadhaa kwenye chart ikiwemo Litawachoma aliyoshirikisha diamond platnumz.

Vanessa mdee $ 3.8 million

Vanessa mdee $ 3.8 million

Japo siku hizi ni Kama aliacha mziki, vanessa mdee ni mmoja wa wasanii tajiri tanzania. Aliwahi kuwa mtangazaji wa MTV base. Ana sauti tamu sana kwa sasa ni mpenzi wa rotimi ambaye ni muigizaji wa power series inayoongozwa na msanii wa marekani, 50 cent.

Alianza mziki tangu mwaka wa 2008 na ashawahi fanya project nyingi na wasanii wengi sana barani afrika. Utajiri wake kwa sasa ni $ 3.8 million dollars

A.Y Tanzania $ 3.5 million

A.Y Tanzania $ 3.5 million

Ni msanii wa zamani kidogo kwani alianza usanii miaka ya tisaini. Kulingana na taarifa za hapa na pale, msanii huyu alianza usanii 1996 ndani ya group iliyojulikana kama S.O.G ila hakukaa sana kwa hicho kikosi kwani mwaka wa 2002 aliamua kufanya kazi peke yake.

Ni Kati ya wasanii walioanzisha bongo flava kitengo Cha hip-hop wakiwemo wasanii kama professor Jay na mwana F.A. Unapoongelea orodha ya wasanii tajiri afrika basi huyu msanii apo katika top ten ya wasanii tajiri Tanzania.

Juma nature – $ 2.1 million

Juma nature - $ 2.1 million

Juma nature ni mwanzilishi wa kikundi Cha temeke kwa jina wanaume halisi. Hii ni kikosi iliyoundwa na wasanii wa mapato ya chini ndani ya dar es salaam. Wanajulikana sana kwa kupiga show ya nguvu sana na unapolipia kwa tamasha yao basi utapata burudani ya kukata na shoka na hautajuta pesa uliyotoa kama kiingilio.

Baraka da prince $ 2 million

Baraka da prince $ 2 million

Japo wengi wanamuona msanii wa kawaida, Baraka da prince ni msanii tajiri na apo kwenye orodha ya wasanii tajiri nchini Tanzania. Anajulikana kuwa na sauti tamu na ana uwezo wa kugeuza sauti yake na kuifanya tamu zaidi.

Dully sykes

Dully sykes

Ni msanii wa zamani sana na Kama kuna wasanii walitengeza pesa nyingi hapo mwanzoni basi dully sykes ni mmoja wa hao wasanii. Ana biashara nyingi sana dar es salaam na pia anamiliki studio yake anapowarekodi wasanii. Japo utajiri wa dully sykes haujulikani, ni mmoja wa wasanii tajiri tanzania.

Soma hii pia ( wasanii tajiri Afrika) je diamond apo kwa list?

Kwa kuwakumbusha tu, hii ndio orodha ya top 10 ya wasanii matajiri tanzania!

 • Diamond platnumz – $ 8 million

 • Harmonize – $ 6 million

 • Alikiba – $ 5.5 million

 • Professor Jay – $ 4.5 million

 • Lady jaydee – $ 4.2

 • Rayvann | Vanny boy – $4.1 million.

 • Zuchu – $ 4

 • Vanessa mdee $ 3.8 million

 • Juma nature – $ 2.1 million

 • Baraka da prince $ 2 million

 • Dully sykes

Soma hii pia ( wasanii tajiri Afrika) je diamond apo kwa list?

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *