MzikiSanaa

Ugomvi wa diamond na harmonize

Ugomvi wa diamond na harmonize umechukua mkondo mpya na kusema kweli wawili hawa wametangaza vita. Wasanii Hawa wawili wako katika orodha ya wasanii tajika ndani ya Sanaa ya tanzania. Mziki wao umepenya ulimwengu mzima na wanajivunia kufaulu kwa mziki wao.

Ushirikiano wa diamond na harmonize.

Historia ya diamond na harmonize.

Kabla ya wawili Hawa kuanzisha ugomvi, walikuwa wakifanya kazi pamoja na kila nyimbo waliyoiachia ilikuwa ikipata mapokezi mazuri. Walikuwa kipenzi Cha watu na ushirikiano wa diamond na harmonize ulileta matunda kwenye sanaa ya tanzania. Wasanii wengi wamekuwa wakifuata nyayo za wasanii Hawa wawili.

Historia ya diamond na harmonize.

Kama umekuwa ukifuatilia Sanaa, wawili Hawa walikutana katika studio alimokuwa akirekodi harmonize. Siku ya kwanza ya diamond kuingia kwa hiyo studio aliweza kuiskiza nyimbo ya kwanza ya harmonize yenye ilikuwa ikitayarishwa. Diamond aliiependa na akamuelezea producer wa harmonize kuwa angependa kukutana na harmonize.

Hii ilikuwa bahati kwa harmonize maana kama unakumbuka vizuri, harmonize alikuwa ashakufa moyo na mziki. Kabla ya harmonize kukutana na diamond, aliwahi kuingia kwenye mashindano ya wasanii yenye huandaliwa Kila mwaka uli kutafuta talanta mbalimbali nchini Tanzania. Majaji walimkoshesha amani harmonize baada ya kumueleza kuwa hana talanta na hatawi enda popote. Hivo tunaweza kusema harmonize kukutana na diamond ilikuwa bahati sana kwake.

Je, ugomvi wa diamond na harmonize ulianzia wapi?

Ushirikiano wa diamond na harmonize.

Baada ya harmonize kuingia label ya wasafi, alifanikiwa kwa mda mfupi sana na mapenzi ya wafuasi wa mziki wake yalizidi. Ilifikia wakati kila mtu alitaka kujua harmonize anapoachilia nyimbo mpya kwani walikuwa na kiu Cha mziki wake. Mziki wake ulizidi kupenya na akaanza kufanya colabo hata na wasanii wa nchi za Nigeria na ulaya. Baada ya mda, harmonize alipata mpenzi Sarah anayesemakana kuwa na hela ndefu sana. Mkewe Sarah anasemekana kutoka kwenye familia ya kitajiri. Habari za hapa na pale zasema kuwa familia yake wanadili na madini mbalimbali kwa hivyo pesa kwao ni kitu ya kawaida.

Mke wa wa harmonize Sarah ndiye alileta ugomvi Kati ya wawili Hawa?

La ama ndio itakuwa ni jibu letu kwa sasa. Sababu ya haya majibu ni kuwa, wakati mwingine mtu akipata pesa huenda akasahau alikotoka. Harmonize kabla ya kumpata Sarah alikuwa mtiifu kwa boss wake diamond na hakuna aliyetarajia kuwa angetoka ndani ya label ya wasafi. Ili kujiondoa kwa label ya wasafi, lazima ulipe gharama za kampuni hiyo ambapo hii kwa harmonize ilikuwa ni kitu rahisi kwani tayari mke wake Sarah angeweza kumsaidia na kiwango chochote cha hela.

Upande wa pili, huenda harmonize aliona ashaanza kudhulimiwa na kampuni ya wasafi na ndio maana akaona ni heri ajitoe na mapema. Wakati mwingine mambo hugeuka na sio kwa kampuni hata kwa familia. Watu huenda wakaanza vizuri lakini baadae watu wakakosana. Tunaweza tukasema makosa ni ya harmonize bila kufikiria kuwa diamond huenda naye alikuwa na mapungufu yake.

Diamond na harmonize watakuja kuelewana?

Mziki ni Kama biashara yoyote ile. Ukiwa na biashara inayofanana na ya mwenzake basi huenda kukawa na kutoelewana Kati yenu kwani Kila mtu anavutia kwake na kila mtu anaiona biashara yake kuwa zaidi ya mwenzake. Diamond na harmonize ni vigumu sana waelewane kwa sasa maana wote wanafanya biashara moja. Harmonize tayari ashaanza kufuata nyayo za diamond na kwa sasa hivi amewasajili wasanii zaidi ya wawili ndani ya label ya konde gang.

Hii inamaanisha harmonize apo tayari kushindana na aliyekuwa boss wake kwa biashara hiyohiyo moja. Ili kufaulu katika biashara yoyote ile, lazima uwekeze na kama kawaida lazima uwe na hela ya kutosha. Harmonize kwa sasa ana huo uwezo wa kumiliki label maana ana hela. Kwa sasa hawezi sema yuarudi kwa diamond na tayari ashaupata utamu wa pesa ya mziki wake ndani ya label yake binafsi.

Nyimbo ya harmonize ‘mshamba’ ilikuwa inamlenga diamond?

Kulingana na uchunguzi wetu, harmonize allimlenga diamond. Kwa video yake pia aliweza kumueka jamaa wenye muonekano kama wa diamond mwenye alikuwa ndani ya swimming pool. Wengi waliongea sana na mafans wa diamond walishikwa na hamaki baada ya kugundua harmonize allimlenga boss wake wa zamani. Diamond  hakuongelea kuhusu hiyo nyimbo japo wengi walitamani diamond aongelee kuhusu mshamba yake diamond.

Soma hii pia ( uhusiano wa Zuchu na diamond platnumz)

 

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *